HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MADIWANI MKOANI DODOMA WAMEWASIMAMISHA KAZI BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO

 Wafanya Biashara za masokoni wakikusanya vitu vyao kwa hofu ili kukimbia baada ya kushtuliwa kuwa asikari wa manispaa wanaokamata watu wanaovunja sheria ndogondogo za manispaa wanakuja kuwakamata katika eneo hilo la stand ya muda ya Daladala ya Oil Com ambapo wamekuwa kero kutokana na msongamano mkubwa wanaousababisha.
Na John Banda,Dodoma.

MADIWANI mkoa wa Dodoma wamewasimamisha kazi  baadhi ya watumishi katika Halmashauri hiyo kwa kushindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuiletea hasara Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Hali hiyo ilijitokeza jana mkoani hapa katika kikao cha dharula cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ambacho kililenga kujadili mapendekezo ya kamati za madiwani katika vyama kuhusu hoja za ukaguzi maalumu .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Meya wa Manispaa ya Dodoma Emmanuel Mwiliko alieleza kuwa baraza limeamua kupitisha kusimamishwa kazi kwa watumishi hao wakiwemo watumishi katika tume ya Uchunguzi wa mchakato wa zabuni ya ushuru wa soko la Saba saba.

Mwiliko aliwataja watumishi hao kuwa ni Mkama Musese ambaye ni Mhasibu wa mapato,Barbanas Ngungo ni mtunza vitabu vya kukusanya mapato,Paulendo Mwasi ambaye ni Kaimu Ofisa Manunuzi na Elias Kamala Ofisa Biashara.

Aliongeza kuwa Watumishi wengine waliosimamishwa ni waliohusika na Uendelezaji wa viwanja vinne vya Halmashauri na Ununuzi wa gari la Halmashauri ambapo Baraza la madiwani halikuridhika na majibu yaliyotolewa na kamati hiyo.

“Kuhusu uendelezaji wa viwanja hivyo vinne imebainika kwamba kuna udanganyifu katika malipo ya fedha ambazo zimekwisha lipwa kwa Mhandisi wa Uendelezaji wa viwanja hivyo kwani katika kikao cha baraza la madiwani majibu yaliyotolewa na Menejimenti yalionesha Mhandisi Mshauri alishalipwa Milioni 49,257,565 wakati usahihi wa ufuatiliaji unaonesha kuwa Mhandisi huyo allilipwa Shilingi 142,898,943.02.
“Kuhusu ununuzi wa gari la Halmashauri iligundulika kuwa Bodi ya zabuni iliidhinisha na kuweka mkataba wa ununuzi huo kwa shilingi 94,130,400.00 badala yake gari hilo lilinunuliwa kwa Shilingi 154,565,250.00 na ongezeko la bei halikupata kibali au idhini ya Bodi ya zabuni wala kikao cha kamati ya fedha na Uongozi”alisema Mwiliko.
Aidha aliwataja wahusika hao kuwa ni Issack Kissa Mchumi wa Manispaa,Richard Chacha Mkuu wa Idara,Ardhi na Mipango Miji,Mukama Musese Mhasibu Daraja la kwanza,Neema Chamgeni Mchumi Daraja la pili na Happiness Matonya Mchumi Daraja la pili.
Hata hivyo Mwiliko alieleza kuwa Baraza pia limependekeza iundwe tume ya Madiwani ikijumuisha vyombo vya dola na wataalamu wa Manispaa ili mkufanya uchunguzi wa masuala hayo pamoja na kupendekezwa kuwa wataalamu watoke TAKUKURU,polisi,Mkaguzi wa nje na Mhandisi wa Ujenzi na sheria.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: