Dodoma. Siku chache baada ya Waziri wa Afrika
Mashariki Samuel Sitta kumhusisha Dk John Magufuli na kundi la urais la
mwaka 2015, Waziri huyo wa Ujenzi, ameibuka na kupinga kauli hiyo,
akisisitiza hafikirii kuwania nafasi hiyo.
Waziri Sitta alinukuliwa na gazeti hili juzi
akieleza kuwa wakati ukifika, yeye na rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk Magufuli
na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, watachagua mmoja wao
watakayeona anafaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Alisema
hayo juzi kwenye Kongamano la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la
wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine
(SAUT), Mwanza.
Kabla ya hapo alikuwa amewataja rafiki zake hao
wakati wa hafla ya kuchangia Kanisa Katoliki, Josephine Bakita, Parokia
ya Igoma, Mwanza, Jumapili iliyopita.
Alisema hatagombea tena ubunge mwaka 2015, baada
ya kuwa katika ulingo wa siasa kwa miaka 35 na badala yake ataangalia
namna nyingine ya kuwatumikia wananchi huku akigusia mchakato wa kuwania
urais ambao alieleza anamwachia Mungu.
“Kwa ubunge nimekwishawaeleza inatosha, sitagombea
tena kwani miaka 35 inatosha, … lakini hatima yangu ni nini siwezi
kujua lakini nina afya nzuri na mmoja wa wanasiasa wakongwe, wenye afya
nzuri, mnaona ninavyopendeza... kwa urais namwachia Mungu tutaona,”
alisema Sitta.
SOMA HABARI ZAIDI KA KUBOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment