|
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bw. Said Mgalula, akimkabidhi kipaza sauti Balozi wa Chapa Vodacom,
Msanii Mwana FA, ili awashushie mistari wakazi wa mji huo waliojitokeza
kwenye kampeni ya uelimishaji jamii kuhusu fistula na kwamba matibabu
yake yanapatikana bila malipo kwenye hospitali ya CCBRT kwa gharama za
Vodacom na Vodafone ya Uingereza. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiteta jambo na MwanaFA kwenye kampeni ya Fistula Inatibika
|
Balozi
wa Chapa Vodacom, Mwana FA, akiwahamasisha wakazi wa Geita kuunga mkono
kampeni ya kumaliza tatizo la fistula ifikapo mwaka 2016 inayofadhiliwa
na Vodacom na Vodafone ya Uingereza kupitia hospitali ya CCBRT. |
|
Balozi
wa Chapa Vodacom, Msanii Mwana FA, akichana mistari mbele ya wakazi wa
Mji wa Geita waliofika katika kampeni ya uelimishaji umma kuhusu fistula
na kusambaza ujumbe wa 'fistula inatibika, jitokeze upate matibabu bila
ua malipo'. Mwana FA yupo kwenye msafara wa kueneza ujumbe huo kwa
mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro na Pwani
kwa ufadhili wa Vodacom. |
|
Meneja
wa Vodacom Mwanza, Victoria na mwenzake wa Misungwi, Gift wakihifadhi
nambari maalum ya kupiga bure 0800752227 kwa masuala yoyote yanayohusu
fistula baada ya kutangazwa kwenye kampeni ya kuwaelimsisha wakazi wa
mji wa Geita kuelekea kilele cha siku ya fistula duniani Mei 23. Nambari
hiyo ni kwa wateja wa Vodacom pekee.Vodacom na Vodafone ya Uingereza
hugharamia matibabu bila malipo kwa wagonjwa wote wa fistula
wanaoitibiwa katika hospitali ya CCBRT. |
|
Muuguzi
na Mnasihi wa CCBRT, Theodola Millinga, akielimisha wakazi wa Geita
kuhusu fistula na namna ya kupata matibabu yake bila malipo kwenye
hospitali ya CCBRT kupitia ufadhili wa Vodacom na Vodafone ya Uingereza.
Zoezi hilo ni sehemu ya kampeni ya kusambaza ujumbe wa 'Fistula
inatibika, jitokeze upate matibabu bila ya malipo' inayondelea mikoani
kwa ufadhili wa Vodacom na Vodafone ikishirikiana na CCBRT. |
|
Mkazi
wa Geita (kushoto), akiuliza swali kuhusu fistula wakati wa kampeni ya
kufikisha ujumbe wa Fistula inatibika jitokeza upate matibabu bila ya
malipo kwenye hospitali ya CCBRT kwa ufadhili wa Vodacom na Vodafone ya
Uingereza. Zoezi hilo ni sehemu ya kampeni ya kusambaza ujumbe kuhusu
fistula inayoendelea mikoani kwa ufadhili wa Vodacom na Vodafone
ikishirikiana na CCBRT kuelekea siku ya fistula duniani Mei 23. |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Geira Said Magalula (katikati), Balozi wa Chapa Vodacom
Mwana FA na Meneja Uhusiano wa Mambo ya nje wa Vodacom, Salum Mwalim
wakifurahia moja ya tukio wakati wa kampeni ya kuelimisha wakazi wa
Geita kuhusu fistula na kufikisha ujumbe wa 'Fistula inatibika, jitokeze
upate matibabu bila ya malipo' iliyoendeshwa mjini Geita ikiwa ni
sehemu ya shughuli za kuelekea siku ya fistula duniani Mei 23. Vodacom
na Vodafone hufadhili matibabu kwa wanawake wenye fistula kwenye
hospitali ya CCBRT. |
|
Shuhuda
wa fistula akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoteseka na fistula kwa mika
minne kabla ya Vodacom kufadhili matibabu yake kwenye hospitali ya
CCBRT. Ushuhuda huo ulitolewa wakati wa kampeni ya kuelimisha wakazi wa
Geita kuhusu fistula na kufikisha ujumbe wa 'Fistula inatibika jitokeza
upate matibabu bila ya malipo'.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi wake kwenye kampeni ya Fistula Inatibika
Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na timu nzima inayoshiriki katika msafara wa Fistula Inatibika
Kampeni ya Fistula inatibika inaendelea kutoka Geita kuelekea Singida kupitia Sengerema kwa kutumia kivuko cha MV Misungwi
|
.............................................
Geita yaguswa na kampeni ya fistula
Katika kuelekea kuadhimisha siku ya Fistula Duniani, 23/5/2013,
Vodacom kwa kushirikiana na taasisi ys CCBRT wameandaa safari ya
kuzunguka nchi nzima inayofahamika kama ‘Fistula Inatibika’ kutokea
Bukoba hadi Dar es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya siku hiyo
kwenye viwanja vya CCBRT yatakayopokelewa na Rais Jakaya Kikwete.
Safari hiyo ambayo inahusisha pia kupita kwenye
sehemu mbalimbali kuwapa wananchi ujumbe kuwa Fistula inatibika,
itajumuisha pia kukusanya ujumbe kutoka kwa familia zilizoathirika na
Fistula kupeleka kwa Rais hapo tarehe 23 ya mwezi huu.
Msafara huo utakaochukua jumla ya siku saba, unaongozwa na
mwanamuziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA,
ambaye atakuwa akiwapa elimu kuhusiana na Fistula wananchi wa sehemu
tofauti tofauti watakaopitiwa na msafara huo.
Picha: Msafara wa Fistula ukiwa Geita
No comments:
Post a Comment