HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI

Mwanafunzi  wa chuo kikuu cha Dodoma  anayejulikana  kwa jina  la Boid Mwakitalima  amefariki dunia  baada  kugongwa na treni na pia wanafunzi huyo  alikuwa  mwaka  wa  tatu.

Taarifa zinaeleza  kuwa, mwanafunzi  huyo  alikuwa   anatembea pembezoni  mwa  reli huku  akiwa ameweka  "headphone"  sikioni, hali  iliyomfanya  ashindwe  kusikia ama  kuhisi  chochote  juu  ya  muungurumo  wa  treni  hilo  mpaka  lilipomsogelea  karibu  na  kumsukuma  pembeni  ambapo  aliangukia  chuma  na  kuaga  dunia  pale  pale.
Jeneza lililobeba mwili wa Boid Mwakitalimalikitolewa kwenye ambulance ya chuo kikuu cha Dodoma
 Makamu Mkuu wa Chuo kikuu  cha Dodoma Prof.Idrisa Kikula  akiwasili Collage ya Informatics
Prof. Idrisa Kikula akipokelea kwenye msiba wa mwanafunzi wa Colllage ya Informatics kwa ajiri ya kuuaga mwili wa marehemu
  Baadhi ya viongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma wakienda kuaga mwili wa marehemu katikakati ni Prof. Idrisa Kikula, mbele  ni Mshauri wa wanafunzi ( Dean of Student) Chuo kikuu cha Dodoma, Nyuma ni mshauri wa wanafunzi, Pro.Anatory  ( Dean of Students)  Collage ya Informatics na Katikati ni Makamu mkuu wa chuo cha Dodoma. Baada  ya  ajali  hiyo, mwanafunzi  huyo  alipelekwa  chumba  cha kuhifadhia  maiti  katika  hospitali  ya  Mkoa  wa Domoma, "General hospital" ambapo  leo  hii  ameagwa  na wanafunzi wenzake  wa  chuo  kikuu  cha Dodoma  na  kusafirishwa  kwenda  nyumbani  kwao Mbeya kwa  mazishi.
Wanachuo wakipokezana jeneza lililokuwa limeubeba mwili wa marehemu Boid Mwakitalima kuonesha upendo kwa mwanachuo mwenzao
 Wanafunzi wakiuaga  mwili  wa  marehemu  kwa  huzuni

Baadhi ya wanafunzi waliofika kuaga mwili wa marehemu Boid Mwakitalima 
 Mkuu wa  Collage ya Informatics, Prof. Mvuma,  akitoa  nasaha  zake
 Rais  wa wanafunzi, Collage ya Informatics  akitoa  nasaha  zake


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: