MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia
kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. Katika hati ya madai
hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group
ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo
zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27
mwaka huu. Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G.
Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha
makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.
-
No comments:
Post a Comment