By: VIJIMAMBO
on May 31, 2013
/
 |
Marehemu Albert
Mangwea enzi za uhai wake
Kama kamati tunaomba kutoa taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert
Mangwea utafika siku ya jumapili ya tarehe 2/06/2013 saa nane mchana na
sio siku ya jumamosi kama ilivyotaarifiwa hapo awali , Sababu za Mwili
wa Albert Mangweha kushindwa kufika jumamosi kama ilivyopangwa ni
kutokana Watanzania wenzetu waishio Afrika Kusini kuomba na wao kutoa
heshima zao za mwisho .
Kwa Maana hiyo basi taratibu zote za kuaga
mwili wa Albert Mangweha kwa Wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya Jirani
zitafanyika siku ya Jumatatu ya tarehe 03/06/2013 kuanzia saa mbili
asubui mpaka saa sita mchana , ambapo baada ya hapo safari rasmi ya
kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi itaanza. Tunaomba radhi kwa
usumbufu wote uliojitokeza Asante
|
Tag:
PAMOJA BLOG's Admin
HABARI, SIASA , AFYA , JAMII NA MATUKIO MBALIMBALI.
No comments:
Post a Comment