Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha CUF kuwa ni chama
cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni,
wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...
Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema
asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge..
Kipengele kinachowasumbua katika hotuba ya Wenje ni hiki hapa...ambacho
kimejaa facts na ukweli. Wakanushe hizi facts. Wajibu hoja si
kumshambulia mtoa hoja. That is what argumentation is all about, let
alone critical thinking.
Kitu gani si cha kweli hapa?
3.0. VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa
‘United Nations University’(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012
iliyoandaliwa na Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani
kutoka nje katika mabadiliko ya kisiasa Tanzania ‘Donor Assistance and
Political Reform in Tanzania’, inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada
kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka
1990-2010.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi
inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka
nje ya nchi na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za
Uingereza, Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na
taasisi kama Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.
Pamoja na misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana
duniani pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila
tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake
tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na
rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada
hiyo.
Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado
vyama vya siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya
siasa katika mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina
mbalimbali kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na
mirengo ya kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo
vyama vya siasa vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea
kutoka nje ya nchi na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza
propaganda za uongo kuwa vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za
magharibi.
Mheshimiwa Spika, CCM wao ‘wanajiita’ kuwa wapo mrengo wa
kijamaa/kikomunisti na wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na
nyenzo kutoka Umoja wa Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni ‘Socialist
International’ kutoka katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP
,Uingereza kupitia chama cha Labour,China kupitia chama cha Kikomunist
,Marekani kupitia chama cha Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na
kiufundi ambayo CCM imekuwa ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi
hadharani hata mara moja kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea
na hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake
za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja
na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni
kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali
ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza,
Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(
www.liberal-international.org)
kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki
ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada,
Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group
cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo
nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na
msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano
na chama cha Kiliberali kutoka Norway.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya
Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni
umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake
mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii,
ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”.
Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika
serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party
cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata
mrengo huo.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote
ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao
na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa
vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .
Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.
Source:Jamii Forums
-
No comments:
Post a Comment