Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoka kufunga Semina ya siku Mbili
iliyofanyika Dodoma jana iliyowahusisha Wabunge, Wakuu wa Mkoa na
Wilaya wa Nchi Nzima Kuhusu Utaratibu mpya wa Utoaji wa Ruzuku ya mbolea
ya mazao kwa Wakulima katikati ni Waziri wa Kilimo na Chakula
Christopher Chiza Naibu Waziri wa wizara hiyo Adamu Malima na Mkuu wa
Wilaya ya Bunda Anjelina Mabula
Washiriki wa Semina ya Utaratibu Mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea Kwa wakulima iliyofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya
ya Bunda Ajelina Mabula nje ya ukumbi wa Loyal Village Dodoma walipoku
wakitoka Kwenye Semina ya wakuu wa mikoa, Wilaya na Wabunge kuhusu Mfumo
mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea ya mazao kwa wakulima, iliyoandaliwa
na Wizara ya kilimo na Chakula.(PICHA NA JOHN BANDA)Washiriki wa Semina ya Utaratibu Mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea Kwa wakulima iliyofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili
Na John Banda, Dodoma
BAADHI ya
Wakuu wa Wilaya hapa Nchini wameonekana kuukataa mfumo mpya wa utaratibu wa utoaji ruzuku ya
pembejeo kwa mikopo kwa wakulima na kudai kuwa mfumo huo hautawasaidia wakulima
bali watanufaika wachache kama yalivyokuwa Mabilioni ya JK.
Wakuu hao wa Wilaya walitoa kauli hiyo jana Mjini hapa wakati wakichangia mapendekezo ya utoaji ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa Wakulima kwa kutumia mikopo .
Mmoja wa Wakuu hao wa Wilaya Anthoni Mataka ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero alisema kuwa mfumo huo kwa wakulima wa kawaida ni tatizo kwani hawawezi kumudu kukopa kutokana na suala hilo kuwa janga na kwamba wakulima hawatanufaika bali watanufaika wachache.
“Mfano mzuri tukumbuke yale mabilioni ya JK nani alinufaika kama sio wajanja wachache ambao ndio walinufaika na fedha zile, ni vyema Serikali ikaliangalia suala hili kwa umakin.”
Aliitaka Serikali kutekeleza mfumo huo mpya wa utoaji ruzuku ya pembejeo kwa mkopo kwa Wakulima kwa majaribio tena kupitia Vyama vichache vya wakulima vya akiba na mikopo (SACCOS) ili kuona kama mfumo huo unafaa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chemba Francis Isaack alionyesha wasiwasi na kutaka kujua Serikali imejipangaje katika ukopeshaji huo wa ruzuku za pembejeo kwa mkulima mmojammoja na mipaka yake.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo alisema kuwa kuhusu mfumo huo Serikali inatakiwa kuwa makini na vilevile ijipange.
“Utaratibu huu mpya wa utoaji ruzuku ni vyema tukawa makini na kukajipanga ili tuweze kuufanikisha kwani ni suala gumu na linahitaji uangalifu.”Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Singida Parseko Kone alionekana kuwa kinyume na wakuu wenzake kwa madai kuwa hivi sasa baadhi ya benki nyingi ni kero kutokana na kuwanyonya wakulima katika utozaji wa riba kubwa.
Kone alitolea mfano wa suala la mazao ghalani kwa Mkoa wake ilikuwa ni tatizo hivyo ni vizuri Serikali ikaliangalia suala hilo kwa umakini wa hali ya juu.
Licha ya Wakuu hao wa Wilaya kuonekana kupinga utaratibu huo baadhi ya Wakuu wa Mikoa wameonekana kushinikiza utaratibu huo utumike na kuwataka Wakuu hao wa Wilaya kutoogopa bali wakatekeleze suala hilo kwa kujiamini.
Kufuatia kuwepo kwa kauli hiyo ya baadhi ya wakuu hao wa Mikoa Mbunge wa Maswa Magharibi(CHADEMA )John Shibuda na kusema kuwa kila mfumo una kasoro zake na anashangazwa na kitendo cha Serikali kushindwa kuondoa kasoro hizo zilizopo katika mfumo wa utoaji ruzuku na badala yake huja na mmbadala ambao sio suluhusho.
“Mara nyingi Serikali ikiona jambo linaharibika huwa inaamua kuja na mmbadala wake badala ya kufanya masahihisho,nilitegemea kabisa hapa tutajadili mapungufu ya mifumo hii ya utoaji ruzuku wa pembejeo lakini sivyo, nasema hivi ukitaka kujikinga na maralia ni vizuri ukaondoa mazalia ya mbu hapo ndo maralia yatakwisha.”Alisema Shibuda.
Warsha hiyo ya siku mbili kuhusu usambazaji wa pembejeo za kilimo imewakutanisha Wakuu wa Wilaya wa hapa nchini,Wakuu wa Mikoa pamoja na Kamati ya Maji,kilimo na mifugo.
Awali,Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Christopher Chiza alisema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa sababu kubwa za uzalishaji mdogo wa mazao ya chakula nchini hususani Zao la Mahindi kupungua na kuwa chini yakilo 500 kwa ekari ni matumizi madogo ya pembejeo bora za kilimo.
Alisema kuwa wakulima wengi nchini wameacha kutumia mbegu bora za kilimo na mbolea kutokana na kuwepo kwa bei kubwa za ruzuku za mbegu bora za kilimo na mbolea kwa wakulima wadogo.
Chiza alieleza kuwa ruzuku kwa wakulima imekuwa ikichukuliwa tofauti lakini walengwa wakubwa wanao takiwa kupata ruzuku hizo za pembejeo za kilimo ni wakulima .
PAMOJAPURE

No comments:
Post a Comment