Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu
wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema leo kwenye
Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa
zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa
wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa
kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na
kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea
Sehemu ya umati wa watu ukiwa
kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda
fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa
hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika nafasi ya kujikwamua
kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa
nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja
vya Nyerere Skwea
Baadhi ya Wasanii wa Filamu hapa
nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake Kajala walikuwa ni miongoni
mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo ya mshikamano yaliyokuwa
yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba jumbe mbalimbali za
kupinga wizi wa kazi sanaa.
Matembezi ya mshikamano ya
kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo,ikiwa sambamba na
kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini .
Waziri Mkuu Pinda akizungumza
mbele ya baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na
watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine wa sanaa waliojumuika kwa
pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada
kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda
fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa
hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga
uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.
Mh.Pinda aliishukuru kampuni ya
Clouds Media Group kwa kazi nzuri walioianzisha ya kuwasaidia vijana kwa
namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwaamsha na kuwafungua
macho na kuwaelimisha namna ya kuziona fursa zilizopo kwa ajili ya
kujikwamua kimaisha,aliongeza kuwa kupitia ujumbe huo wa MADE IN
TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga ratiba nzuri ya kuliendeleza
zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha taasisi nyingine zikiwemo za
serikali katika kuhakikisha jambo hilo linaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema
Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika kwenye viwanja vya Nyerere
Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda.
Baadhi ya magari yakiwa
yamesimama yakipisha matembezi ya mshikamano yaliyokuwa yakielekea
kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana.
Baadhi ya Watangazaji wa clouds
FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya/tasnia ya filamu na
wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa pamoja kwenye viwanja vya
Nyerere Skwea mapema leo mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh
Waziri Mkuu Pinda.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni na
Mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini,Mh.Idd Azan akiunga mkono harakati za
kupapambana na maharamia wa kazi za sanaa hapa nchini
Gari ya Waziri Mkuu Pinda ikiwasili
Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na
Naibu Waziri wa Habari,Vijana, michezo na Utamaduni,Mh.Amos Makala
habari,Michezo mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea
mapema leo mchana mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na
Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba
mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo
mchana mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Pinda akiwasili
kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,mjini Dodoma mapema leo mchana huku
akiwapungia mkono baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu
pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wananchi wengine kwa ujumla
waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo
mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali
iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa
upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba
na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,pichani kati ni
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akimkaribisha.
Mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Jahazi,Wasi Wasi Mwambulambo akiserebuka na Mh.Rehema Nchimbi.
Baada ya muda kulipita burudani ya pamoja ya mchanganyiko kama hivi safi kabisa kabla ya Waziri Mkuu kuwasili viwanjani hapo.
Pichani
kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,kulia mtangazaji wa
Clouds FM Mbwiga Mbwiguke na Shaffih Dauda (shoto) wakitwibiwirika kwa
pamoja mapema leo mchana mjini Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere skwea.
Mh.Waziri Mkuu Pinda akizungumza
jambo na Muimbaji mahiri wa mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto.Kulia ni
Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba na
kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Chamwino,Mh.Fatma Ally akishuhudia
mazungumzo hayo.
Waziri
Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa
Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake
mpya ulioitwa TWENZETU kwa minajili ya kuielimisha jamii kuwa na
tabia ya kupenda vya kwao na kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN
TANZANIA kujikwamua kimaisha.
Waziri
Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii (wote
waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo
mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia
wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya
ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao
kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA .
No comments:
Post a Comment