HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » YALIYOJIRI LEO KWENYE KIKAO CHA WASANII KUHUSU MAZISHI YA MAREHEMU ALBERT MANGWEA

 Kaka wa Merehemu Albert Mangwea(katikati) akiwa na dada yake (kulia)
Adam Juma alichaguliwa kama mzungumzaji wa kamati hiyo ambapo ametoa taratibu zote watakazofanya wao kama kamati ambapo amesisistza watu kushirikiana kwani msiba ni wetu sote hakuna mwenye mamlaka ya kuhodhi bali ni makubalino ya familia ndio yataendesha shughuli nzima
Mwanamitindo Flaviana Matata (kushoto) akiwa na Sajjo(katikati) pamoja na Mwana FA(kulia) wakijadili jambo baada ya kamati kupewa mamlaka ya kusimamia masuala yote ya muziki
Hii ndio kamati ikiongozwa na P Funk ambayeni mkuu wa kamati na wasanii wengine walioko kwenye kamati hii ni Wasaanii wa Chemba Squard (Noorah na Mez B), Jay Moe, Lady Jadee, Professa Jay, Micheli Mzungu, Rommy Jones,  Madam Juma na T.I.D Chizi Mox

Profesa Jay akijadiliana jambo na wenzake kwenye viwanja vya leaders leo jioni
Wadau waliofika kwenye viwanja vya leader club leo

Dada wa marehemu Albert Mangwea akizungumza na waandishi wa habari
Kala Jeremiah amemwelezea Ngwea kama msanii wa pekee alikuwa 100% mkali wa Free Style na alimpenda kwa nyimbo kali kama Ghetto langu iliyom inspire kuingia kwenye Game.
  Mwana FA amesema ni vitu vingi vya kukumbuka kutoka kwa Ngwea lakini kikubwa ni uwezo wake wa kuandika na mashairi yake kutojirudia hadi akatoa mfano kuwa mara nyingi alikuwa akimwambia Ngwea kwamba ana Range anatembea nalo kichwani lakini Ngwea alimjibu kuwa si Range moja tu bali mawili anamiliki kichwani kwake so tunaweza kuona jinsi gani alikuwa mtu muhimu kwenye game.
 Miliki wa blog wa Pamojapure (kushoto) akiwa na wasanii wa Bongo fleva ili kujua kinachoendelea kuhusu masuala yote ya msiba waMarehemu Albert Mangwea
 Ndugu, Jamaa na marafiki wa msanii Albert Mangwea wamekutana leo jioni kuanzia saa kumi jioni maeneo ya Leaders Club kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu msiba huo ikiwa ni kuangalia kwa pamoja kile wanachoweza kufanya kwa pamoja na taratibu nzima ikiwemo michango kuhusu msiba mzima. 


PAMOJAPURE BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: