HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » AJALI ZA BODABODA ZINAUA ZAIDI MKOANI DODOMA




Na John Banda, Dodoma
JUMLA ya watu 19 wamepoteza maisha kati ya Januari na June mwaka huu kutokana na ajali zilizosababishwa na uzembe wa madereva  wanaondesha Bodaboda.
Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alipokuwa akifungua mkutano kati ya jeshi hilo na waendesha Bodaboda uliofanyika katika Bwalo la Polisi kwa lengo la kutatua changamoto ya Ajali za mara kwa mara.
Kamanda Misime alisema katika kipindi hicho jumla ya ajali 48 sawa na asilimia 18.7,  zilitokea na kati ya ajali hizo 17 zikiua watu 19  na nyingine 31 zikisababisha majuruhi 47 walioachwa na ulemavu wa kudumu, huku ajali 42 zikiwa zimesababishwa na Waendesha Bodaboda boda.
Kamanda huyo aliongeza kuwa kama mtu akisikia idadi hiyo wamepoteza maisha kwa anaweza kuona ni ndogo lakini ni kibwa kutokna na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
‘’Vifo vya watu 19 kwa upeo wa Binadamu unaweza kuona wachache lakini ni kubwa ukizingatia zimesababishwa na uzembe na vimepunguza nguvukazi na kuwaacha wategemezi wengi wakiwa na shida zaidi ya walizokuwa nazo wakati waliyekuwa wakimtegemea alipokuwepo hai’, alisema Misime
Aidha aliwataka madereva hao wa Bodaboda kutumia nguvu kubwa ya kuzingatia sheria za Barabarani kama wanavyokuwa na ushirikiano wakati wanapokuwa misururu wakati wakimsindikiza dereva mwenzao aliyepoteza maisha kwa ajali kutokana na uzembe.
Alisema ni vizuri washirikiane katika kuhakikisha wanazingatia sheria na kutoa kipaumbele kwa watumiaji wengine wa Barabara ili waweze kupita huku wakiongozwa na alama za husika zilizopo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: