Kamanda wa Polisi (RPC) wa Mkoa wa Dodoma, David Misime (katikati), alipokuwa na kikao na Viongozi wa Madhebu ya Dini ya Ki-Islamu na Wakristo aliowaita Ofisini kwake kwa Mazungumzo ya Mahusiano Mema ili kukomesha Ajali, Mauaji, na Vitendo Viovu mkoani humo.
Na Bryceson Mathias
‘Mshale kwenda Msituni haukupotea!’
INGAWA waswahili husema, “Mshale kwenda msituni haukupotea”, hivi karibuni Usemi huo ulibadilika, ambapo Shekhe wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Said Kitilla, alitofautiana kimtazamo na Mkuu wa Polisi (RPC), David Misime.
Shekhe Kitilla alitofautiana kimtazamo na Mesime katika kikao cha mahusiano ya ujirani mwema, ambapo Polisi iliwaangukia Viongozi wa Dini ikiwaomba washirikiana kubaini Uhalifu na Wahalifu, ambao wengi ni Waumini wao.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Nia ya Misime kwa viongozi wa Dini aliwaita kuwataka wajenga mahusiano ya pande hizo mbili (Polisi na Viongozi wa Dini), ili katika mahubiri yao wawaonye waumini wao, kuachana na vitendo viovu vinavyosababisha Maafa na Vifo mkoani.
Alivitaja Vitendo viovu vinavyosababisha Maafa na vifo kuwa ni pamoja na Kuendesha Bodaboda na Magari Kasi, Utumiaji wa Vilevi, Madawa, Ngono Zembe, Ukahaba na Mambo yanayofanana na hayo.
Ilieleza Vitendo hivyo vinasababisha Vifo, Ulemavu, Wizi, Ujambazi na Uharibifu wa Mali na Maisha ya watu, jambo ambalo alidai, Viongozi hao wa Kidini wakitumia Doria yao ya Kiroho, na Polisi wakatumia Doria yao ya Kimwili,Amani na Usalama nchini vitakuwepo, na uharifu utapungua.
Misime aliwataka Viongozi wa Dini waendelea kuhubiri Utii wa sheria bila shuruti, kutokana na wao kuwa karibu na wananchi kwa kuwa watu wakiitii sheria hiyo, hata ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa uovu huo, zitapugua.
“Mimi ninawaheshimu viongozi wa dini kwa kuwa mnachangia utulivu na Amani nchini, na hata mkiniona na kosa, msisisite kunionya kama mlivyofanya zamani bila kuongopa cheo cha mtu”alisema Misime.
Misime aliwaonya baadhi ya askari Polisi wasio waamnifu wanaovujisha siri ambazo wananchi wametoa kuhusu uharifu na waharifu na kudai, ili kudhibiti tabia hiyo askari watakaobainika watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Mchungaji Kanisa la Moroviani Iringa Road, Kaminyoge Andendekisye, alisema mahusiano kati ya Jeshi hilo na viongozi wa Dini, yalikuwa mabovu kutokana na kutotambuliwa na kupuuzwa kama hawana uwezo wa kuleka hali ya utulivu katika Jamii.
Ustadhi Musa Juma alisema, kukaa na Polisi kunafanya watambuane na kufanikisha utendaji wa kazi na kuuweka mji mfano wa Utulifu na Amani, lakini ukafuatiwa na Mbunge Machali NCCR-Mageuzi kuvamiwa na Majambazi.
Viongozi wa Ki-Islam na Kikristo waliahidi kutoa ushirikiano wa kuhubiri ombila la RPC kwa waumini wao, lakini Shekhe Kitilla alitofautiana na wenzake akidai Serikali ndiyo inaendekeza uharifu na Uovu ulioshamiri nchini.
Kitilla alinukuu Mbinu alizotaja aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Tabora, Morogoro na Mlezi wa Klabu ya Wandishi Morogoro (Moro Press Club), Stephen Mashishanga, kuzuia Askari kutumia Nguvu wanapofautiana na Wananchi, alipohojiwa na TBC1 karibuni.
Kitilla alisema,“Viongozi wa Dini tukikemea Pombe, Serikali inatoa Vibali vya Ulevi Baa, Viosk, zinazonywewa toka asubuhi na Kazi hazifanyiki. Tukizuia Kondom, Serikali inaruhusu, Tukikemea Mavazi yasiyo na heshima, Serikali iko kimya!
“Tukikemea Michezo Michafu ya TV, Mavazi Nusu Uchi hasa Urembo na Miziki, Serikali inatoa Ruksa, Tukikataza Ulevi, Sigara Serikali inaanzisha Viwanda vyake.
“Tunampigia Mbuzi Gitaa! Serikali Hasikii!’ alisema Shekhe Kitilla ambaye hivi karibuni kwenye Mtandao wa Habari Mseto Blog, alipinga kuwa CHADEMA si Chama cha Kikabila, Kidini au Kiukanda, akijinadi yuko tayari kujiunga nacho, maana kina ukweli.
No comments:
Post a Comment