1. Ngwar ana hits nyingi sana
Nilizungumza na Jay Mo aliyesema tangu Ngwair afariki ndio amegundua kuwa alikuwa na hits nyingi zake na alizoshirikishwa pengine kuliko msanii yeyote nchini
2.Ngwair ana mashabiki wengi
Umati uliojitokeza uwanja wa ndege kupokea mwili wake, watu wa kila rika waliojitokeza Leaders Club kuuaga na nyomi la uwanja wa Jamhuri Morogoro ni jibu tosha.
Leo June 7, Cpwaa ameandika kupitia Facebook: One day I will share this experience. During mazishi ya kaka yangu Ngwair kuna mUda nilItafuta chemba kuvuta fegi pale makaburini. Kuna Bibi moja,akaomba chupa yangu ya maji nimpe nikimaliza(Alikuwa anakusanya chupa tupu za vinywaji) nikamwambia ntampa nikimaliza, nilivyomaliza fegi akaniuliza sasa hivi saa ngapi? nikamuambia saa 9 kasoro..akasema “Mangwea anakaribia”, dakika 25 baadaye mwili wa marehemu ukafika pale, Baada ya kusubiri karibu masaa matatu toka niwahi makaburini sababu uwanjani ilikuwa nomaa, palikuwa hapatoshi.
Nashukuru nilipata hata nafasi ya kubeba jeneza dakika za mwisho, Only if my brother was brought back for few minutes to see the love he had from his people. Nimesukuma watu,mpaka watoto nimewafukuzuka watoke eneo la tukio, it was too crazy, Kweli M2 wa watu! BodaBoda ndio usisemee. Am sure if he saw it, he smiled…” WASANII tumeonyesha ushirikiano mzuri sana! Big Up to kamati na wadau wote. Huu muziki tunaudai na uko powerful kuliko politics behind it. Let this be a SPARK.”
3. Bongo Flava ni muziki wenye heshima
Mazishi ya Mangwair yamekuwa kama ya kiongozi mkubwa wa nchi kiasi kilichomfanya Jaydee aseme hiyo ni ‘Power of Bongo Flava wakati Nikki Mbishi akitweet: Ukiangalia picha za umati uliojitokeza kumlaki Ngwea ndo utajua wasanii tunatakiwa kuwa MATAJIRI kiasi gani. Naye Soggy Doggy jana alitweet, “Umati uliomzika Mangwea leo ni fundisho kubwa kwa wasanii,wadau na serikali kwa ujumla,tupigane umati uendane na kipato chetu.TUSAIDIENI.
4. Wasanii wana umoja
Msiba wa Ngwair umeonesha jinsi ambavyo wasanii wana umoja pale panapotokea matatizo. Kama wakijikusanya hivi kudai haki zao dhidi ya wizi wa sanaa, muziki utakuwa na faida zaidi.
5. Kila msanii wa hip hop anamheshimu Mangwea
Kila msanii niliyeongea naye alikuwa haachi kukisifia kipaji alichokuwa nacho Mangwair. Uwezo wake wa kufreestyle na kuandika mashairi makali umewafanya wana hip hop wote wa Tanzania wampe salute!
6. Tuwe na kasumba ya kuwasifia wasanii wangali wakiwa hai wajijue wanavyokubalika
Kama sifa hizi anazopewa sasa Mangwea angekuwa anapewa angali akiwa hai, huenda mambo yangekuwa tofauti. Radio zote za Tanzania zingempa promo aliyoipata kipindi cha harakati ya mazishi yake leo hii Ngwair angekuwa anapiga show zenye hela kama Diamond, lakini tumeshachelewa.
7. Msanii asaidiwe mapema pale anapoonekana ana tatizo
Mangwair alikuwa msanii mmoja tu kati ya wasanii wengi waliopo kwenye wakati mgumu sana licha ya uwezo wao mkubwa kwenye muziki. Wapo wasanii wengi tu tunafamu wamejiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwasababu mbalimbali, wasaidiee kungali mapema. Baada ya kifo cha Ngwair, Mwana FA aliandika: Unabaki unajilaumu…unahisi kuna vitu ungesema/ungefanya pengine mwana angekuwa na pumzi bado…RIP hommie….Surname ya freestyle.
7. Hip Hop sio uhuni
Kama unahisi Hip Hop ni uhuni basi huenda hujahudhuria mazishi ya Mangwea. Watoto, vijana, wazee, matajiri, maskini, viongozi na watu wa kila aina, wamejitokeza kwa wimbo kuuaga mwili wa Ngwair kuanzia Johannesburg, Dar es Salaam na Morogoro. Kama Hip Hop ingekuwa uhuni mambo yasingekuwa hivyo.
8. Umoja kwa vyombo vya habari unaweza kuupeleka muziki wa Tanzania mbali sana
Clouds Media Group, East Africa TV/Radio, Times FM, Entertainment Masters na vyombo vingine vya habari viliweka ushindano wao pembeni na kuungana pamoja kufanikisha mazishi ya Mangwea, si jambo dogo. Fikiria kama siku moja vyombo hivyo vikiungana pamoja kufanya tamasha la pamoja (si kwa ajili ya kupata faida) kuwapa burudani wananchi wa miji kadhaa nchini? I’m just saying!!!
Mawili ya mwisho na mengine nikuachie wewe msomaji, umejifunza nini kutokana na msiba wa Ngwair?
SOURECE: BONGO 5
No comments:
Post a Comment