Hata
hivyo cha kushangaza mwandishi wetu alikuta bendera ya Taifa ikishushwa
saa moja jioni hali wengine wakiendelea na shughuli zao hapo shuleni
Siku
chache mara baada ya Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa katika
shule ya secondari Hollywood iliyopo wilayani Momba mkoani Mbeya. Ndugu Amina
Mwamkinga (20) kutimuliwa shule takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa
anajihusisha na imani za Kishirikina ameendelea kusota mtaani huku akishindwa
kujua nini hatma ya maish yake ..
Mara baada ya kupokea kwa taarifa hiyo
Afisa Elimu Wilaya ya Momba Ndugu Izack Mgaya alilazimika kumuita
Mkuu wa shule hiyo kwa lengo la kupata maelezo ya kina juu ya kuwepo kwa
sakata hilo la mwanafunzi kufukuzwa shule .
Mkuu huyo wa shule hiyo Ndugu Imani Mtafya
ambaye mara baada ya kuitwa na afisa elimu huyo alikili kutokea kwa
sakata hilo la mwanafunzi ambapo alieleza kuwa licha ya mwanafunzi
kutuhumiwa kwa ushirikina hakupatiwa nafasi ya kujieleza juu ya yeye kutuhumiwa
kwake na vitendo vya ushirikina na uongozi wa shule hiyo.
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa pande
zote mbili afisa Elimu aliagiza mwanafunzi huyo kupatiwa uhamisho kwenda
shule nyingine ili aendelee na masomo yake licha ya mwanafunzi huyo kusimama
kuendelea na masomo yake kwa kipindi cha miezi mitatu sasa.
Hata hivyo baada ya mwanafunzi huyo kufika
shuleni hapo kwa lengo la kupata uhamisho huo alielezwa na uongozi wa shule
hiyo ya Hollywood kwamba picha zake pamoja na taarifa nyingine zimepotea
hivyo kufanya mwanafunzi huyo kutapatapa na kutofahamu nini
cha kufanya.
Kufuatia hali Amina Mwamkinga ambaye ni mlemevu
wa ngozi (Albino) ameziomba asasi mbalimbali pamoja na
serikali kumsaidia ili kufahamu hatima ya maisha yake ya baadaye pamoja na
kutoa wito kwa jamii kutambua kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanahaki ya
kupata elimu kwa watu wengine hivyo wasiwatenge .
Machi
9, Mwaka huu wanafunzi wa shule hiyo walimtuhumu binti huyo kujihusisha na
vitendo vya kishirikina ambapo uongozi wa shule hiyo uliamua kumtimua
mwanafunzi huyo bila kupata maelezo ya kina.
Mhanga
wa tukio hilo Amina Mwankinga amesema tangu kipindi hicho alipofukuzwa
bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali
iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi
asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri
kama Shuka nk.
Amesema
kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua
yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo baada ya kukosa msaada ambapo
alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
Binti
huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini Dar Es Salaam
ameomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo
kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
Naye
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale amesema alikuwa
halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye
juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za
malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.
Awali
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema
kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa
anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea
ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi
aendelee na masomo kama kawaida.
Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment