.jpg)
Chief wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akimuonyesha Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini DKT David Malole Historia ya kabila la kigogo iliyoandikwa kwenye Mnara uliojengwa pembezoni mwa kisima Cha Maajabu Kilichopo katika mlima Wa Bwibwi kijiji cha Iyumbu, wakati wa tambiko la wazee wa kabila hilo.(PICHA NA JOHN BANDA)

.jpg)
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini DKT. David Malole akishuka ngazi kuingia kwenye Kisima cha Maajabu Kilichopo katika mlima wa Bwibwi uliyopo katika kijiji cha iyumbu Mbunge huyo ni Miongoni mwa watu 100 walioingia kwa pamoja kukishuhudia kisima hicho wakati wa tambiko la wazee wa kabila hilo.
.jpg)
.jpg)
Chief wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akiwa juu ya Mnara uliopo pembezoni mwa Kisima cha maajabu kilichopo katika mlima wa Bwibwi kijiji cha iyumbu manispaa ya Dodoma, uliondikwa hitoria ya kabila hilo wakati wa tambiko la mwaka huu ambalo hufanyika kila katikati ya mwaka.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini DKT. David Mchiwa Malole akimiminiwa Pombe ya Kienyeji na Mke wa Chiefu wa kabila la kigogo Luce Masuma Chihoma, kwaajili ya tambiko la kabila la kigogo lililofanyika katika kisima cha maajabu kilichopo katika mlima wa Bwibwi kijiji cha Iyumbu kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.
.jpg)
Na John Banda, Dodoma
Mbuge wa Dodoma Mjini DKT David Mchiwa Malole [CCM] Amsema ataishawishi Serikali ili itenge eneo la makumbusho ya kitaifa Mkoani Hapa Hususani katika Mlima wa Bwibwi .
DKT. Malole aliyasema hayo alipokuwa amehudhuria Sherehe za Tambiko la kabila la kigogo lililofanyika pembezoni mwa kisima cha maajabu kilichopo katika mlima wa Bwibwi katika kijiji cha Iyumbu.
‘’Hivi sasa Mji wa Dar es salaam una msongamano mkubwa sana, la msingi serikali ione umuhimu wa kuweka makumbusho Dodoma kwa sababu ni makao makuu na watu wa kila mkoa watakaotaka kuyatembelea na kujifunza itakuwa rahisi kwao’’, alisema.
Aidha Dkt. Malole Alisema eneo hilo ni eneo zuri na la kihistoria kutokana na kuwa na kisima cha maajabu ambacho pamoja na watu zaidi ya 30 kuzama na kupoteza maisha na nyimbo, ngoma na vigelegle vyao kusikika hata leo bado kina njia ya kuingilia Bahari ya hindi.
Hivyo la msingi eneo hilo litunzwe na kuenziwa maana hata wananchi wanaotumia maji yaliyopo katika kisima hicho hujisikia vyema, wakikumbuka ndugu zao waliopoteza maisha kwenye kisima hicho kilichomeza watu zaidi ya 100 wakati akikikagua.
Mbunge Huyo aliongeza kuwa wengi wameacha mila na destuli za makabila yao hata kufikia kutowafunza watoto wao Lugha za kwao kama vile kabila la kigogo, sukuma, Kinyamwezi, kihehe, kidigo na makabila yote nchini kutokana na ukisasa unaoletwa na utandawazi.
Awali Mkuu wa kabila la kigogo Chief Lazaro Chihoma alisema lengo lao kama Serikali itawasikiliza na kuwatengea eneo hilo watahakikisha wanawavuta watu mikoa mingine ili waje wajenge nyumba za kiasili pamoja na kuleta tamaduni zao.
Chihoma alisema kitajengwa chuo ambacho kitafundisha na kuwakumbusha vizazi vijavyo kuhusu mila na Destuli za makabila ya kitanzani, kwa kutumia wakuu wa kamila wa makabila yote yatakayokuwa yamejumuika pamoja kufundisha na kuendeleza tamaduni husika.
‘’Utandawazi umekuja kutupotezea tamaduni zetu, hebu ona vijana wa kike na wakiume wanavyotembea wakiwa wamebana na kuyaonyesha maumbile na wengine wakitembea wameshusha nguo kama wanataka kujisaidia kumbe wanatembea hayo yote tutakuwa wakali tutawakamata na kuwachapa viboko’’, alisema Chief Chihoma.
No comments:
Post a Comment