WANASEMA maji ni uhai, kinyume chake bila maji hakuna uhai wa
mwanadamu na hata wanyama. Kimsingi kauli hii inaonesha umuhimu wa maji
katika maisha ya kila siku ya binadamu na hata viumbe wengine.
Shughuli nyingi zinazofanywa na mwanadamu kila siku zinategemea uwepo
wa maji. Matumizi ya maji kwa shughuli za binadamu hayaepukiki. Na hata
katika mwili wa binadau ni muhimu zaidi, kama huto yaitaji maji kwa
kunywa utayahitaji kwa kuoga na usafi wa shughuli nyingine.
Kwa mantiki hiyo hali yoyote ya upatikanaji ngumu ya upatikanaji wa
maji unaathiri maisha ya kila siku ya mwanadamu. Shida ya huduma ya maji
eneo fulani huweza kuchangia ugumu wa maisha kiasi fulani. Shida ya
maji maeneo mengine huweza kupunguza shughuli za uzalishaji mali, hii ni
kutokana na muda mwingi kupotezwa na jamii kwa ufuatiliaji wa maji hasa
maeneo ya vijijini.
Hali kama hii ya shida ya huduma ya maji ndiyo inayowakumba wananchi
wa vijiji anuai vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Kata ya Kishapu ina vijiji nane yaani Mhunze, Lubaga, Isoso, Mwanuru,
Migunga, Mwamagembe, Mtaga, na Kishapu yenyewe.
Japokuwa vijiji vingi vina shida kubwa ya huduma za maji, lakini hali
ya ugumu wa upatikanaji huduma hizo hutofautiana kutoka kijiji kimoja
hadi kingine. Kati ya vijiji vyote nane vijiji vinne ndio vyenye shida
ya maji zaidi. Vijiji hivyo ni pamoja na Lubaga, Isoso, Mwanuru na
Kishapu yenyewe.
CHANZO: THE HABARI
No comments:
Post a Comment