WAZIRI MKUU AWAAGIZA WATENDAJI WAKE KUJENGA MIUNDOMBINU YA MAJI KATIKA VIJIJI VITANO(5) MKOANI DODOMA


Na John Banda, Dodoma
WAZIRI Mkuu  Mizengo Pinda amewaagiza Wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha ujenzi wote wa miundombinu ya maji katika vijiji 5 unakamilika ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.
Aliyasema hayo alipokuwa akifungua Mafunzo kuhusu mfumo mpya wa Ufuatiliji na Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, iliyowahusisha watendaji hao wa Serikali Mjini Dodoma jana.
Aliwataka wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ili Miundombinu hiyo ya maji katika vijiji 5 vya mwanzo inakamilika katika kipindi hicho cha miezi 3 mpaka sep 2013 na baada ya hapo Miradi ya maji katika vijiji 5 vitakavyo baki ikamilishwe ifikapo June 30,2014
Pinda alisema ujenzi wa miradi ya maji vijijini inawataka wananchi kuchangia Gharama za uendeshaji na matengenezo baada ya ujenzi kukamilika.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa

‘’Niliagiza na ninasisitiza kuwa michango hiyo ya wananchi isizidi Asilimia 2.5, ya thamani ya maji vijijini uhamasishaji wa uchangiaji ufanyike sambamba na ujenzi wa miradi na usisimame hata kama hata kama wananchi hawajakaimilisha michango yao’’, alisema Pinda.
Aidha Waziri Mkuu Pinda alizitaka Sekretarieti za mikoa zisimamie utoaji wa takwimu sahihi zinazoonyesha hali halisi ya huduma zinazopatikana na pia zinatakiwa kutoa ushauri wa kiufundi pale inapoona kazi hazifanyiki ipasavyo.
Pinda aliongeza kuwa watendaji hao ngazi ya mikoa na wilaya wahakikishe Fedha zote zilizoongezwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini zinawekewa mfumo ambao utahakikisha zinatumika katika malengo yaliyopangwa na ijengwe kati viwango vinavyokubalika si vinginevyo.
Alitananbaisha kuwa Halimashauri zina jukumu la kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuanzisha vyombo huru vya watumiaji maji kwa kutumia sheria ya maji na usafi wa mazingira Na 12 ya mwaka 2009 maana jukumu la usajili wa vyombop hivyo na lao.
‘’Halimashauri zote zihakikishe kuwa miradi yote inatoa huduma ya maji na mingine mipya itakayojengwa kuanzia sasa inaudwa na vyombo vya watumiaji maji’’, alisema
aAliongeza kuwa Halimashauri zote kwa kushirikiana na Sekretarieti za mikia zifuatilie kwa ukaribu utendaji wa sekta binafsi ili kama kutakuwa na uzembe katika utekelezaji wahusika wachukuliwe hatua za kisheria hata ikibidi mikataba yao kusitishwa na kuwaondoa kwenye orodha ya makampuni yaliyoruhusiwa kufanya kazi hapa nchini, wakandarasi wote wa ujenzi wa miundombinu ya maji watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia ubora unaostahili na kwa wakati.

No comments

Powered by Blogger.