MTOTO AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI DAR

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo


Mtoto aliyefahamika kwa jina la Lina Krisantus(4), amefariki baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara katika maeneo ya Tegeta kwa ndevu jijini Dar es Salaam.

Akidhibitisha kutokea kwa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillious Wambura, alisema mtoto huyo alifariki baada ya kugongwa na gari lenye namba T 670 ANF aina ya Benz lililokuwa likitokea Tegeta Kibaoni kuelekea darajani.

Alisema dereva wa gari hilo hakuweza kufahamika kwani alikimbia baada ya ajali na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyama na juhudi za kumsaka dereva huyo zinaendelea.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini

Aidha, katika tukio lingine moto umeteketeza nyumba ya vyumba kumi na vyoo viwili pamoja na mali zote zilizokuwamo ndani ya nyumba hiyo, zenye thamani ya Sh milioni 15 juzi jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema nyumba hiyo iliyoko maeneo ya Kigamboni Southen Beach ambamo wanaishi wafanyakazi wa kampuni hiyo, iliteketea majira ya saa 9.


Alisema chanzo cha moto kinasadikiwa kuwa ni moto uliokuwa umewashwa kwa ajili ya kuchoma taka na moto huo kusambazwa na upepo na kusababisha cheche zilizoruka kwenye paa la nyumba hiyo na kuiteketeza ingawa hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu. 
CHANZO: NIPASHE

No comments

Powered by Blogger.