Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Magreth Zziwa akimsikiliza mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania,Shyrose Bhanji wakati wakielekea bungeni
Spika akiongoza kikao cha jana mchana ambacho kiliahirishwa baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje.
Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge hilo jana kupinga wabunge wenzao wanaoshinikiza hoja zao kwa kutoka kwenye vikao vya bunge hali inayoshusha hadhi ya Spika,bunge na wabunge wenyewe,kutoka kushoto ni Mh.Twaha Taslima,Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Abdula Mwinyi na Nderakindo Kessy
Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini
Mbunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari yalipo makao makuu wa Afrika Mashariki jijini Arusha baada ya kutoka nje na kikao kuhairishwa hadi leo
Kiongozi wa baraza la Wawakilishi Zanzibar,Ali Mzee(kulia)akizungumza na wabunge wa Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA)kutoka kushoto ni Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Nderakindo Kessy,Mh.Twaha Taslima na Mh.Abdula Mwinyi.
Mbunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki,Makongoro Nyerere(kushoto) akifurahia jambo na Mbunge Peter Mathuki aliyewasilisha hoja ya kutaka vikao vya bunge vifanyike kila mwanachama na sio Arusha pekee yalipo makao makuu ya EAC.
Maafisa wa bunge wakitafakari baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje na Spika kuhairisha kikao hadi leo.
No comments:
Post a Comment