CDA WATAKIWA KUTOINGIA KIJIJI CHA IYUMBU, MKOANI DODOMA


 Diwani wa kata ya Iyumbu manispaa ya Dodoma Hezeron Kudugwa akiwafafanulia jambo wananchi wa kata hiyo kwenye mkutano waliokutana kuijadili Barua ya CDA kuhusu kutakiwa kuanza kulipia viwanja.
 Mwenyekiti wa kijiji hicho cha iyumbu Yona Ngobito akielezea jambo kwenye mkutano wa wananchi kuhusu fidia walizolipwa na CDA kwenye mashamba yao na kuwataka kulia viwanja walivyowapa kinyume na makubaliano.
 Wananchi wa kijiji cha Iyumbu manispaa ya Dodoma wakiwaa kwenye mkutano wa wananchi wote ili kuijadili barua ya CDA iliyowataka kuanza kulipia viwanja walivyopewa na mamlaka hiyo baada ya mashamba yao kupimwa.(Picha na John Banda)

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini

Wananchi wa kijiji cha Iyumbu manispaa ya Dodoma wakiwaa kwenye mkutano wa wananchi wote ili kuijadili barua ya CDA iliyowataka kuanza kulipia viwanja walivyopewa na mamlaka hiyo baada ya mashamba yao kupimwa.



Na John Banda, Dodoma
Wananchi wa kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma wameadhimia kuipiga marufuku mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] kutokanyaga katika kijiji chao mpaka makubaliano ya Fidia na kiwanja cha bule yatakapotekelezwa.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi hao baada ya kusomewa barua ya CDA iliyowataka viongozi kuwatangazia wananchi kulipia viwanja walivyopewa wakati wa upimwaji wa maeneo ya mashamba.
Akiongea kwa jazba kwenye mkutano huo mmoja wa wananchi Andason Daudi alisema imefika wakati CDA wapigwe marufuku katika kijiji hicho cha iyumbu kwa sababu hawana faida na wananchi bali waliingia ili kuwaelekeza kwenye umasikini.
Daudi alisema haiwezekani kwenye vikao mamlaka hiyo ilivyofanya nao walipewa ahadi mbele ya mbunge na kaimu mkuu wa wilaya Geradi Guninita, kuwa wakubali mashamba yao yapimwe watapewa fidia na viwanja viwili kama sehemu ya fidia hiyo kwa heka,  sasa hatuwataki.
“Kana mtu akikosea kuna msemo wa kigogo unasema Nyunga ne nzila, kwamba kuna mnyama anaitwa nyunga huwa hatakiwi kuvuka njia akivuka tu hufa, hivyo nawaambia CDA maruku kukanyaga iyumbu mpaka walekebishe usemi wao sisi hatulipii hata sumni’’, alisema Daudi
Kwa upande wake Enest Mahodanga alisema kitendo cha CDA kuwabadilikia na kusema mwananchi anatakiwa kulipia kiwanja kimoja ni kosa, kwa sababu mapatano yalikuwa wananchi watapewa fidia na kiwanja na kama wakitaka kiwanja cha pili  itabidi kilipiwe.
Mahodanga anasema kitendo hicho ni sawa na unyang’anyi wamevamiwa na kunyang’anya mashamba yao kinyume cha utaratibu, hakuna chochote watakacholipwa mpaka makubaliano mapya yafanyike na CDA hawataruhusiwa kaufanya lolote kwenye kijiji hicho.
Nae Diwani wa kata hiyo ya Iyumbu Hezeron Kudugwa alisema CDA inamakosa mengi kwa sababu hata kwenye upimaji na utaji wa fidia pamoja na wananchi kulipwa milion 1 na wengine 3 bado kuna waliolipwa Shl 100, 000 na wengine 700,000.
Kudugwa alitoa mfano wa nyumba ya kawaida tofauti na ya kisasa mtu alilipwa 1.1mil huku ikiwa imejengwa kwa mabati 20 fidia hiyo haikuzingatia hali ya maisha ya sasa na kutengeneza mfarakano kati ya viongozi na wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Yona Ngobito alisema waliwaita CDA ili kuhudhuria mkutano huo ili wawafafanulie wananchi kuhusu mabadiliko ya makubaliano nao kabla ya kupima Ambapo hawakufika kuwasikiliza wananchi.
Ngobito anasema waliamua kuwaita CDA kutokana na kuona kwenye orodha ya majina ya wenye mashamba kuna ulipiaji  wa viwanja kwa skwea mita moja shl 4200 kinyume na makubaliano ya mkutano uliofanyika kwa mkuu wa wilaya Novemba 2,6. 2011  kabla ya upimaji huo kuanza.
“tulika vikao mara mbili vilivyoshirikisha ofisi ya mkuu wa wilaya aliyewakilishwa na Guninita CDA wenyewe na manispaa iliyowakilishwa na chacha na mbunge malole na tukaambiwa Bodi imekubaliana kuwe na fidia na kiwanja kama sehemu ya fidia’’, alisema Ngobito
Ngobito aliongeza kuwa yeye ni kiongozi hivyo ni lazima awasikilize wananchi wake na maamuzi yamekuwa hayo ya kuwaita CDA kama hawatafika kutoa ufafanuzi kwa wananchi hakutakuwa na kitakachoendelea toka mamlaka hiyo kijijini hapo.

No comments

Powered by Blogger.