WAZIRI WA KILIMO NA USHIRIKA ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE MKOANI DODOMA


Waziri wa Kilimo chakula na ushirika Mhandisi Christipher Chiza, Mwenyekti wa uandaaji ya maonyesho ya wakulima[TASO] Engrbert Moyo na Mtoto Nunu aliyeambatana na Waziri Chiza wakitembea katika viwanya vya Nanenane wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya wakulima kitaifa yanayofanyika Dodoma.
 Waziri Chiza akikaribishwa kuangalia kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani kwa wananchi waliokuwa wakisubili hotuba ya uzinduzi wa  maonyesho ya wakulima katika viwanja vya nanenane Nzuguni Dodoma.


Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini



  
 Ofisa kilimo, uzalishaji na Mbegu wa Wilaya ya Chamwino  Aithan Chaula akimuelezea jambo Waziri wa Kilimo na Chakula Mhandisi Christopher Chiza katika viwanja vya nanenane alipotembelea banda hilo kabla ya kuzindua rasmi maonyesho hayo juzi. 
 Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akikagua Bustani za mbogamboga na matunda za Taasisi ya Magereza zilizopo viwanja vya nanenanea Dodoma na aliongozana Kamishna wa Magereza anaeongoza Divisheni ya Urekebishaji Wafungwa Deonice Chamlesile na mkuu wa mkoa  Dr. Rehema Nchimbi 

 Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akiangalia tunda aina ya Bilinganya kwenye banda la wilaya ya chamwino alipotem,belea kabla ya kuzindua maonyesho ya wakulima nanenane yaliyoanza tarehe 1 na yanatarajia kuhitimishwa Agost 7 kutokana na sikukuu ya idd kuangukia nanenane.
 Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akagua bustani ya nyanya kwenye maonyesho hayo ya nanenane. 

No comments

Powered by Blogger.