Khalid akinyanyuliwa juu kwa kifaa maalum Kutokana na unene, ukubwa na uzito wake, Khalid hawezi kutembea wala
kusogea mwenyewe bila msaada wa kifaa maalum cha kuongea na kumbeba
akiwa katika kitanda chake. Khalid ana umri wa miaka kati ya 18 na 20.
Mfalme Abdullah amelipia ndege maalum kumchukua Khalid Mohsin Shaeri iliyomchukua kumpeleka hospitali.Kijana
huyo hakuwahi kuondoka chumbani mwake kwa kipindi cha miaka miwili na
nusu. Sehemu ya nyumba yao imevunjwa ili kuweza kumshusha kutoka ghorofa
ya pili kilipokuwa chumba chake.
Mfalme aliaigiza Shaeri atibiwe
miezi sita iliyopita lakini matibabu yalichelewa hadi pale kitanda
maalum kingetengenezwa nchni Marekani.
Wizara ya afya ya Saudi Arabia imeshirikiana na jeshi la wananchi na Red Cross ili kumtoa ndani mgonjwa huyo.
Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini
Kutokana na rekodi za Guinness, Manuel Uribe kutoka Mexico ndiye
aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mzito na mnene zaidi duniani ambapo
alikuwa na uzito wa kilo 560. Baada ya kuonekana na kuingizwa katika
matibabu, kwa sasa amepungua na kufikia uzito wa kilo 444.
Khalid akipelekwa kwenye ndege ili apelekwe hospitalin
Source: CNN na Daily Mail
No comments:
Post a Comment