Mbunge
wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, ameliambia Bunge
kuwa majengo na viwanja vingi vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi
(CCM), havilipiwi kodi ya majengo.
Msigwa alitoa kauli hiyo alipokuwa akiuliza swali la nyongeza bungeni jana.
“Majengo ya CCM na viwanja vingi havilipiwi kodi ya majengo kwa mfano pale Iringa mjini jengo la CCM limekuwa halilipi kodi,”alisema.
Alihoji kama hiyo ni sera ya CCM kuwatoza watu wengine kodi lakini yenyewe hawajitozi kodi.
Akijibu swali hilo baada kusita kwa muda mfupi hali iliyowafanya wabunge wa kambi ya upinzani kupiga makofi, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema serikali haichagui mtu wa kumtoza kodi.
“Hizo ni 'interest' zako kuhoji kuhusiana na majengo ya CCM lakini wako wengi ambao hawalipi kodi, ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wote wanalipa na hata nyumba yako kuhakikisha inalipa kodi,”alisema.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Katika swali la msingi, Mbunge wa Tumbe, (CUF), Rashid Ali Abdallah, alitaka kufahamu ni watu wangapi wanaotegemea kulipa kodi? Wangapi hawalipi kwa kuzingatia idadi ya Watanzania milioni 43.9 Tanzania Bara.
Akijibu swali hilo, Mkuya alisema hadi kufikia Julai 31 mwaka huu, idadi ya walipa kodi waliosajiliwa kwa kupatiwa namba ya mlipa kodi ya mapato (TIN), walikuwa 1,199,942.
Alisema kwa upande wa idadi ya watu wanaolipa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni 21,659 na kwamba idadi hiyo haijumuishi wafanyakazi wanaokatwa kodi moja kwa moja kutoka kwa waajiri wao.
Aidha, alisema jumla ya waajiri 92, 510 wanawasilisha kodi za watumishi wanayokatwa kwenye mshahara ya lipa kadiri unavyopata (PAYE).
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment