Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume akizungumza mapema leo kwenye semina ya FURSA kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha.
Mkurugenzi
wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya
Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja
Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na
Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa
vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa
Mtwara.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa
makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana
iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpo ambaye pia ni mwanachama wa NSSF,akizungumza fursa mbalimbali alizozipata ndani ya shirika hilo la NSSF,mbele ya wakati lukuki wa mji wa Mtwara waliojitokeza kushiriki semina hiyo,iliyokuwa na mafanikio makubwa.
Baadhi ya akina mama wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semini hiyo
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.Katika semini hiyo vijana wemejitokeza kwa wingi.
Msanii wa Kughani mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na Wana wa Mtwara kuhusiana na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa huu,kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika leo mkoani humu.
Baadhi ya Waendesha Bodaboda walipata wasaa wa kuacha kazi zao na kushiriki semina ya Fursa kwa Vijana.
Baadhi ya vijana wakiwa nje wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikiendelea ukumbini
CHANZO: JIACHIE BLOG
CHANZO: JIACHIE BLOG
No comments:
Post a Comment