Utafiti mpya umebaini kuwa wanaume hukosa amani pale wapenzi wao ama wake zao wanaofanikiwa zaidi. Utafiti huo umeonesha kuwa kujiamini kwa mwanaume kuna uhusiano na mafanikio ya wenzi wao. Hata hivyo, hali haiko hivyo kwa wanawake ambapo wao hawaathiriki na mafanikio ya wapenzi wao zaidi ya kufurahia.
Utafiti huo umechapishwa mtandaoni na kwenye jarida la Personality and Social Psychology. Umesema kuwa mwanaume hutishika pale mchumba wake anapomzidi katika jambo walifanyalo kwa mfano hata wanapojaribu kupunguza uzito.
Umebaini kuwa wanaume automatically hutafsiri mafanikio ya wake zao kama kufeli kwao hata kama si washindani wao wa moja kwa moja. Utafiti huo ulifanywa kwa watu 896 katika majaribio matano.
No comments:
Post a Comment