Askari wa kikosi cha usalama
Barabarani akichukua maelezo kwa mmoja wa majeruhi wa basi la Al Saedy Express lenye namba za usajili T433 BLR lililogangana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mahindi kupeleka Dar es salaam.
Daktari
wa Mifipa wa hospital ya Rufaa ya Dodoma Maitundo Stanley akimhudumia
mmoja wa majeruhi wa ajali iliyohusisha Basi la Al Saedy Express lililokuwa
likitoka Dar es laam kwenda Dodoma na Lori la mizigo uso kwa uso na
kusababisha vifo vya watu 6.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kaimu
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Damas Nyanda akitoa ufafanuzi kuhusu
ajali iliyohusisha basi la Al Saedy Express na Lori la mizigo na kusababisha
vifo vya watu 6 na wengine 17 kujeruhiwa vibaya ikiwemo kuvunjika viungo
mbalimbali vya miili yao.
Mmoja
wa majeruhi wa basi la Al Saedy Express lenye namba za usajili T433 BLR lililogangana uso kwa uso na
lori lililokuwa limebeba mahindi kupeleka Dar es salaam akisaidiwa na
ndugu yake

Na John Banda, Dodoma
MWENDO kasi wa 140 aliyokuwa akiutumia Dereva wa Basi la Al
sayd Expess ulisabisha vifo vya zaidi ya watu 6 akiwemo yeye na dereva wa lori
alilogongana nalo na wengine 17 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa
ya Mkoa .
Ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha chinangali 2 wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati basi
hilo lenye namba za usajili T 433 DLR
lililokuwa likitokea Dar es saam kuja mkoani hapa lilipogongana uso kwa uso na
lori hilo lenye namba za usajili T102 CGR aina ya Layland Daf lilikuwa na tera.
moja wa majeruhi wa ajali hiyo Juma Yusuph 31 mhehe mkazi wa Chidachi manispaa ya Dodoma alisema
mwendo huo ulibadilika na kuwa mkubwa kuanzi walipotoka mkaoni Morogoro kiasi
cha kufikia kasi hiyo.
‘’Mimi nilikuwa nimekaa mbele karibu na dereva nilipochungulia
nikaona speed inasoma 140 huku jamaa
akiyapita magali ya mizigo zaidi ya 4 kwa pamoja kama unavyoona mimi
nimevunjika mguu lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa Yule dereva ni kama
alipanga kujiua na kweli nilishuhudia baadhi ya viungo vyake mbele ya lori’’,
alisema yusuph.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao wengi wao walivunjika viungo
vikiwemo miguu na mikono walisema mwendo mkubwa uloanza baada ya kutoka Morogoro
Kaimu kamanda wa polisi mkoa Damas Nyanda aliwataja majina
waliopoteza maisha mbele ya wandishi wa
habari kuwa Dereva wa lori Hassan Mohamed umri kati ya 30,35, Ahmed Said, Husen
Rajab, Imran Sharif wakazi wa Dar, na Dereva wa Basi hilo Nizar Akran Khan
mkazi wa Mpwapwa wakati mwili wa marehemu
mmoja bado haujatambuliwa.
Kaimu kamanda huyo alisema Alisema Miili ya maremu
imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Dodoma na wengine 17 waliojeruhiwa kulazwa wakiwemo 7 wanawake na
wanaume 10
Nyanda alisema chanzo
cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2.30 usiku wa juzi jumapili
ni Mwendo kasi wa Dereva wa Basi hilo ambapo ashindwa kulimudu wakati akijaribu
kusimama ili kujaribu kujiepusha na ajali
hiyo.
Jeshi hilo la polisilimetoa wito kwa watumiaji wa barabara
kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani huku wakiwa natahadhali ya kujua kuwa
kuna watumiaji wengine.






No comments:
Post a Comment