Chief Lazaro chihoma (wa pili kutoka kulia) akiwaongoza Mbunge wa jimbo la Dodoma
mjini DKT David Malole(wa tatu kutoka Kushoto), Katibu Mwenezi wa CCM wilaya Salum Kalli, mjumbe
wa ya siasa wa wilaya CCM Judith Myeya na viongozi wengine kuona sehemu
ya ikulu ya kimila ilivyohalibiwa na CDA.
Mbunge wa Dodoma Mjini DKT David Malole ambae ni mjumbe wa Bodi ya CDA
akionyeshwa miti na mabaki mengine na Mtemi Lazaro Chihoma namna
makumbusho hayo ya kimila yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi
yalivyobomolewa na CDA.
Mtemi Lazaro Chihoma Akiwaonyesha baadhi ya watu akiwemo Mbunge wajimbo
la Dodoma mjini DKT David Malole na waCCM waliofika kuona jinsi
makumbusho hayo ya kimila yalivyovunjwa na CDA.(Picha na John Banda)
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Mtemi wa makumbusho ya kimila Lazaro Chihoma akitoa tangazo la kuendelea
na ujenzi kwa mala nyingine mbele ya waandishi wa habari siku mja tangu
makumbusho hayo yaliyopo katika mlima wa Bwibwi kubomolewa na mamlaka
ya ustawishaji makao makuu CDA.
Mjumbe wa Bodi ya mamraka ya usitawishaji makao makuu [CDA] DKT David
Malole akijadiliana jambo na Mtemi wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma
[kulia] na Mzenge tumbi Andason Chaulema kwenye makumbusho ya kimila
yalibomolewa na Tinga tinga la CDA chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mjumbe wa Kamati ya siasa CCM Wilaya ya Dodoma Judith Myeya akifafanua
jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mala baada ya kujionea
jinsi makumbusho ya kimila ya kabila la kigogo yalivyobomolewa na
Mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA, na kupendekeza mamlaka
hiyoifutwe.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha iyumbu akiendelea na ujenzi wa moja
ya nyumba za matambiko ya kimila kwa kabila la kigogo siku moja baada ya
CDA kufika na kubomoa nyumba hizo zilizojengwa kwa miti juu na chini
bila kujali kisima chenye kumbukumbu za kihistoria kilichopo katika eneo
hilo.
Na John Banda, Dodoma
MBUNGE wa Dodoma Mjini Mhe, Dkt. David Malole amejitoa Rasmi kujihusisha na Bodi ya mamlaka ya ustawishaji makao makuu [CDA] kutokana na kutoshirikishwa katika maamuzi mbalimbali. Mbunge huyo alichukua uamuzi huo wakati alipofika kujionea bomoabomoa
iliyofanywa na mamraka hiyo, baada ya kubomoa vibanda vya makumbusho ya wagogo vilivyopo mlima Bwibwi.
Dkt. Malole alisema Hawezi kuendelea kujiona mjumbe katika bodi hiyo wakati hashirikishwi kwenye maamuzi mbalimbali yakiwemo ya upangaji wa mji huo na kubwa zaidi wakati mamraka hiyo inapopanga kwenda kubomoa
nyumba za watu.
Aliongeza kuwa yeye kama mbunge na aliyechaguliwa na wananchi Hawezi kuendelea kuvumilia kuona wakionewa kwa kufanyiwavitendo vya kinyama vya kuvunjiwa tena hata bila ya kusikilizwa.
“Mimi kama mjumbe wa Bodi ya CDA, Sijashirikishwa hivyo nakubaliana na hoja za wananchi wanazosema kuwa watendaji wa mamraka hiyo akiwemo mkurugenzi wananidharau,
“Mahudhurio yangu kama mjumbe kwenye bodi hayana maana yoyote nikienda sithaminiwi , hivyo kuanzia leo najitoa, Siwezi kuendelea kuwa mjumbe wa Bodi ambayo inanyanyasa wananchi’’, alisema Malole
Aidha Dkt Malole alisema yeye kama mbunge CDA haifai na kuishauri serikali kuwa ni afadhali majukumu waliyopewa mamraka hiyo yahamishiwe Halimashari ya manispaa hiyo ambayo inaweza kutekeleza majukumu hayo bila kubuguzi wananchi wake.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha makumbusho ya kimila cha Bwibwi [Mzenga itumbi] Andason Chaulema alisema wafanyakazi wa CDA walifika katika eneo hilo palipo na Kisima cha maajabu wakiwa na Tinga tinga, huku wakiwa na polisi zaidi ya 10 na walipofika waliiga risasi 3 hewani. Chaulema alisema baada ya watu kutawanyika kukimbilia mapolini yeye alibaki kuwasikiliza baada ya kuona wapo na watu wa CDA, wakmuuliza kibali cha kujenga nyumba za makumbusho hayo aliposema wamsubili Mtemi wao Lazaro Chihoma wakakataa na kuanza kubomoa nyumba hizo
zilizojengwa kwa miti juu na chini.
Nao viongozi wa Chama cha mapindizi [CCM] wilaya ya Dodoma mjini Katibu Mwenezi Wilaya Salum Kalli na Mjumbe wa kamati ya Siasa [W] CCM Judith Myeya walisema kuhifadhi makumbusho ya kimila ni sera ya chama hicho iliyopo kwenye ilani ya 2010/15.
Kalli aliongeza kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na CDA ni vya kukidharirisha na kukiondolea chama imani kwa wananchi wake na kuahidi kulifikisha kwa mwenyekiti Jakaya Kikwete ili aiangalie upya mamlaka hiyo kama ina haja ya kuendelea kuwepo la sivyo watawashawishi wananchi ili wapige kura za maoni ili kuikaa.
Kisima cha maajabu kilichopo katika Mlima huo wa Bwibwi kilivumbuliwa na Mbwa aliyekuwa na kiu ya maji aliyemtoroka muwindaji [Mpelembi] aliyekuwa akiwinda pembezoni mwa mlima huo miaka ya 1850 na kutawazwa kuwa mtemi wa kitongoji hicho baada ya kuhamia kutoka na kupata maji yaliyowasaidi watu wa kipindi hicho.
No comments:
Post a Comment