Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyata amewaomba wakenya kuwa watulivu wakati huu
ambapo vikosi vya usalama vinafanya jitihada kuhakikisha watu waliobaki
kaitka jengo la WEST GATE wanaokolewa huku akisisitiza kuwa serikli yake
itapambana na magaidi popote pale walipo.
Rais
Kenyatta ametoa kauli hiyo wakati akihutubia taifa jana juu ya tukio
la kuuwawa kwa watu wapatao 68 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa,ambapo
alitoa hotuba hiyo mbele ya ya viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo
aliekuwa waziri mkuu wan chi hiyo raila odinga. Aidha rais uhuru
kenyatta amesema vita hii haihusu dini yoyote wala kabila lolote bali
ni vita ya ugaidi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Tukio
hilo limetokea tangu jumamosi sept 21 ambapo mpaka sasa bado kuna watu
wameshikiliwa na wavamizi hao ndani ya jengo hilo la WEST GATE MALL
lakini serikali ya kenya imewahakikishia wananchi kuwa inafanya jitihada
zote kuwaokoa watu walioko ndani ya jengo hilo.
Hali ilivyokuwa katika Jengo la WEST GATE MALL
CHANZO: ITV TANZANIA





No comments:
Post a Comment