HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » RUSHWA YA NGONO TATIZO KUBWA NCHINI

Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (Tawja)  kimesema rushwa ya ngono  bado ni tatizo kubwa ambalo limeshamiri katika ofisi nyingi hapa nchini.

Mwenyekiti wa chama hicho, Angela Kileo  alisema hayo  jijini Dar es Salaam jana wakati wa warsha ya wadau wa utoaji haki na utokomezaji wa matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.
Alisema baadhi ya waajiri wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kuomba rushwa ya ngono na kuahidi kutoa ajira, kupandisha cheo, au kuongeza posho.
Alisema waathirika wakubwa wa  tatizo hilo ni wanawake maofisini, viwandani, mashuleni, vyuoni, majumbani na sehemu nyingine za uzalishaji na utoaji huduma.


Alisema vitendo hivyo vimekuwa  vikifanyika kwa usiri mkubwa na kwamba licha ya kuwadhalilisha wanawake, lakini pia vinawaathiri kimwili na kisaikolojia.


Kileo aliongeza kuwa, licha ya athari zinazowapata kutokana na tatizo hilo, lakini wengi wao huogopa kuripoti katika vyombo husika kwa kuhofia kupoteza ajira.
Alisema kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa, kuna kila sababu ya kuangalia kuboresha sheria ili kuwalinda wanawake,  pamoja na jamii kushirikiana  katika kutokomeza tatizo hilo.

CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: