Mwakilishi
wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali
yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina
ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi
wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Meneja
wa NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa
mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu
mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa
mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Maxmalipo,Bernard Munubi
akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana
na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia
huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Africans
dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
Sehemu ya meza kuu ya watoayo mada wakishangilia jambo.
Wakifuatilia
kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya
kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.
Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.
Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. 

Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.
PICHA ZOTE NA JIACHIE BLOG
PICHA ZOTE NA JIACHIE BLOG


















No comments:
Post a Comment