Aliyekuwa Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansour Yusouf Himid akizungumza katika kongamano la wazi lililoitishwa na Kamati ya Maridhiano Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipovuliwa uanachama wa CCM. Picha na Talib Uss
Zanzibar. Kamati ya Maridhiano imetoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutaka Zanzibar ijitegemee karibu kwa kila kitu.
Maeneo inayotaka yaondolewe kwenye Muungano ni
uraia na uhamiaji, sarafu na Benki Kuu, mambo ya nje na usajili wa vyama
vya siasa.
Kamati hiyo inayounga mkono muundo wa muungano wa
Serikali tatu inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo,
iliwasilisha mapendekezo hayo juzi katika Ofisi za Tume ya Mabadiliko ya
Katiba na kusema kuwa maoni hayo ndiyo mawazo ya Wazanzibari wengi.
Mapendekezo hayo yalisomwa na Mwakilishi wa Mji
Mkongwe ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Ismail Jussa katika
Kongamano la Katiba lililoandaliwa na kamati hiyo.
Msimamo wa kamati hiyo unaelezwa kuwa chanzo cha
mmoja wa wajumbe wake, Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uanachama wa CCM,
Agosti 26 mwaka huu.
Akisoma mapendekezo hayo, Jussa alisema kwa kuwa
Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar uliziunganisha nchi
zilizokuwa huru, unatakiwa kuitwa Muungano wa Jamhuri za Tanzania,
kusisitiza kuwa rasimu hiyo inatakiwa kueleza wazi kwamba nchi nyingine
zinaweza kuingia kwenye muungano huo.
Endelea kusoma habari hii kwa ubofya hapa chini
Alisema kamati hiyo imependekeza kuwa mambo ya nje yasiwe suala la muungano na badala yake nchi washirika zisimamie zenyewe eneo hilo.
Endelea kusoma habari hii kwa ubofya hapa chini
Alisema kamati hiyo imependekeza kuwa mambo ya nje yasiwe suala la muungano na badala yake nchi washirika zisimamie zenyewe eneo hilo.
Alisema kwa kuwa muungano umetokana na nchi mbili
zilizokubali kuungana na kuunda shirikisho, msingi wa uraia wa
shirikisho utokane na msingi wa mtu kuwa raia wa nchi mshirika na si
kinyume chake.
“Kila nchi mshirika (Zanzibar na Tanganyika),
ibakie na uraia wake na mtu kuwa na uraia wa nchi mshirika ndiko kumpe
uhalali wa kuwa raia wa shirikisho,” alisema.
Pia kamati imependekeza Rais wa muungano ambaye
atakuwa na madaraka ya juu katika shirikisho lote kwa mambo yote ya
Muungano, hivyo nchi washirika zinapaswa kuwa na haki sawa katika kutoa
watu wa kushikilia Baraza la Mawaziri la Muungano, Bunge na Mahakama.
Alisema rasimu inatakiwa itamke wazi kwamba urais
wa Muungano utashikwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya nchi washirika
yaani Tanganyika na Zanzibar na kwamba Rais atangazwe mshindi baada ya
kupata kura zaidi ya asilimia 50 kutoka Tanganyika na Zanzibar.
Alisema badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa
Makamu wa Rais kupatikana kutokana na mgombea mwenza, marais wa nchi
washirika (Zanzibar na Tanganyika) moja kwa moja wawe makamu wa kwanza
na makamu wa pili wa Rais wa Muungano.
Mambo ya kuondolewa
Alisema uchumi si suala la Muungano hata katika
Katiba ya sasa na kwamba nyenzo za kuendeshea na kusimamia uchumi wa
nchi kwa maana ya sera za fedha na uchumi zimeendelea kudhibitiwa
kupitia Serikali ya Muungano.
“Vyombo vikuu vinavyosimamia sera hizo ambavyo ni
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara
ya Fedha ya Serikali ya Muungano vimekuwa vikifanya uamuzi na
kuyatekeleza bila ya kuzingatia kuwa Zanzibar inategemea uchumi wa
utoaji huduma na haiwezi kuwa sawa na uchumi wa Tanganyika ambao
unategemea rasilimali,” alisema.
Akizungumzia usajili wa vyama vya siasa alisema
Rasimu ya Katiba haipaswi kujumuisha suala la vyama vya siasa katika
mambo ya Muungano na kwamba Zanzibar na Tanganyika zinatakiwa
kuandikisha vyama vyake vya siasa.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment