Redd’s
Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (19) akipozi kwa picha
mara baada ya kuibuka mshindi wa taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kutinga
nusu fainali za Miss Tanzania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29
katika shindano hilo dogo kuelekea fainali za Redd’s Miss Tanzania 2013.
Mrembo Happiness Watimanywa akiwa amekubwa na butwaa baada ya kutajwa Mshindi wa Redd's Miss Photogenic 2013.
Redd’s
Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipozi kwa picha
na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya kumsaka mshindi wa taji la
Miss Photogenic 2013. Kutoka kulia ni Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara
Bayo na Jacline Luvanda.(Picha na Father Kidecu Blog)
Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini
Warembo wengine Walioshiriki shindano
hilo wakifuatilia utangazwaji wa matokeo hayo katika Hoteli ya Giraffe
Ocean View katika kambi yao.
Mrembo wa
Mkoa wa Dodoma, na mwakilishi wa Kanda
ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji la Redds Miss Tanzania Photogenic
2013 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano
la Redds Miss Tanzania 2013.
Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo
itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika
kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.
Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss
Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga
picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka
magazeti ya Serkali Daily News, Habarileo na Spotileo.
Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya
tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha
wa Jambo Leo Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.
Dalili za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata
kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja
majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake
ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa
kwashangwe.
Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo
huo ni pamoja na Anastazia
Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness Watimanywa
aliyeibuka mshindi.
Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena
katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu,
katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.
Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na
washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent,
Miss Personality na Miss Sports Woman.
Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na
mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na
Kanda ya Ziwa.
Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania
zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Septemba 21,2013.
No comments:
Post a Comment