HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » DOGO JANJA APIGWA CHINI MTANASHATI, OSTAZ JUMA ADAI HANA NIDHAM

 Dogo Janja
Hatimaye Dogo Janja ametimuliwa kwenye kampuni ya Mtanashati Entertainment kwa kile ambacho Mkurugenzi wake, Ostaz Juma amekitaja kuwa ni kutokana na rapper huyo wa Arusha kuwa mtovu wa nidhamu, kukataa kusoma shule na kutoonekana nyumbani anapokaa kwa muda mrefu pamoja.
Akizungumza na Bongo5, Ostaz alisema ameamua kumfukuza Dogo Janja kutoka Mtanashati baada ya kugundua kuwa atampa matatizo halafu baadaye wazazi wake waje kumtupia lawama.
“Nimemfukuza Dogo janja kwasababu hana heshima,amekimbia nyumbani, anakoishi sikujui ,nimemtafutia shule amekataa kusoma yaani kwa kifupi simwelewi na mimi ni mzazi ambaye nimekabidhiwa kumlea. Kwahiyo kama amenishinda ninamrudisha kwa baba yake tusije tukapeana lawama,” amesema Ostaz.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Bongo5 ilimtafuta Dogo Janja ambaye alisema ni kweli amefukuzwa ila sio kwasababu ya utovu wa nidhamu wala kutomsikiliza Mkurugenzi wake.
“Ostaz ana matatizo yake, naye ni binadamu kama binadamu wengine kwahiyo mimi nasema amenifukuza ila sio kwa sababu ya kuvuta bangi wala kuhama nyumbani kwake na wala sijakataa kusoma shule. Ningependa tuliache hili swala mpaka tutapokutana kifamilia ndipo tutajua sababu aliyonifukuzia ila sio hizo alizozitaja,” amesema rapper huyo.
Kwa upande wake wa Baba mzazi wa Dogo Janja, Abubakari Chande alisema hajui nini kinaendelea Dar es salaam na kama akipata taarifa kutoka kwa Ostaz mmiliki wa Mtanashati atakuwa na cha kuongea lakini kama akiwa kimya basi bado ataendelea kutambua Dogo Janja yupo Mtanashati.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: