HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » PETE YA UCHUMBA YA KIM KARDASHIAN ALIYOVISHWA NA KANYE WEST INAKADIRIWA KUWA NA THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI

 
 Pesa sio kikwazo linapokuja swala la Kim Kardashian na North West kwa rapper Kanye West ambaye wiki hii ameendelea kuudhihirishia ulimwengu juu ya mapenzi ya dhati kwa baby mama wake kwa kumvisha pete ya uchumba yenye thamani kubwa.
Jumatatu (Oct 21) ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Kim Kardashian aliyefikisha miaka 33, katika siku hiyo muhimu boy friend wake na baba wa mwanae Kanye West aliamua kumpa surprise ya maisha baada ya kumvisha pete ya uchumba ikiwa ni miezi 18 toka uhusiano wao uwe hadharani.
Inavyoonekana kidole cha ndoa cha Kim K kimeshazoea kuvishwa pete za thamani kubwa sababu pete aliyovishwa jumatatu na Kanye inakadiriwa kuwa na thamani ya dola million 1.6 (sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2, Kwa mujibu wa Tobias Kormind, ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa 77 Diamonds, aliyeiambia Mail Online.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

“Kim’s ring from Kanye looks like a 15 carat diamond Cushion cut. As its name suggests, the Cushion cut is a rectangular or square shape, with rounded corners that resemble a pillow. It’s very similar looking to the Emerald cut which [ex-husband] Kris Humphries gave her. I would have presumed that Kanye would have been keen to get her a different shape of ring this time, which is possibly why he chose the Cushion cut. I would estimate that a diamond of this size and quality would be worth well over £1 million; Kim is a very lucky woman!”. Alisema
 
Hata hivyo inadaiwa kuwa pete ambayo Kim alivishwa na aliyekuwa mume wake wa zamani Kris Humpheries pia ilikuwa na thamani kubwa ya dola milioni 2 ikiwa ni zaidi ya aliyomvisha Kanye ambayo ni dola milioni 1.6.
Thamani ya pete sio ‘guarantee’ ya kudumu kwa ndoa ndio maana licha ya pete ya Humpheries kuwa na thamani kubwa lakini ilidumu wa siku 72 tu!
Hii itakuwa ni ndoa ya tatu kwa Kim Kardashian na ya kwanza kwa rapper Kanye.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: