Kuna mchezo mchafu unaendelea katika mitandao ya kijamii!! Hackers wameiingilia akauti za Profesa Jay za facebook na Twitter na kuandika kuwa ataperform katika show itakayofanyika katika viwanja vya Leaders, Dar es salaam.
Professor Jay has a show on 2013-10-26 at 18:00 @ Leaders Club in Dar es Salaam http://t.co/g0Yclit1W1 #concert
— Joseph Haule (@Profesa_Jay) October 25, 2013
Akiongea na Gadner G. Habash kwa njia ya simu, Profesa Jay amesema haelewi chochote kuhusu tangazo hilo lilichoandikwa kwenye akaunti hizo. “daah, jamaa wabaya hao, wameshaingilia akaunti yangu.” Amesema Profesa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFA HAPA CHINI
Binafsi nimepata nafasi ya kuongea na Profesa Jay kupitia simu ya Gadner, ambapo aliniuliza maswali kuhakikisha kama kweli ni akaunti zake, na baada ya kumueleza na kugundua ni yake,ameeleza kuwa akaunti yake ya Twitter alikuwa ameiunga na ile ya facebook hivyo itakuwa wamepata access ya zote.
Muda mfupi uliopita, Profesa ameandika kupitia akaunti hiyo hiyo ya twitter:
ATTENTION: Kuna mtu amehack account yangu ya Twitter na FB na kutangaza Kuwa nitakuwepo kesho kwenye FIESTA DAR, Taarifa hizo hazina UKWELI!
— Joseph Haule (@Profesa_Jay)




No comments:
Post a Comment