HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » DKT SENGONDO MVUNGI AVAMIWA NA KUJERUHIWA VIBAYA NA WATU WASIOJULIKANA USIKU WA KUAMKIA LEO JIJINI DAR

Dkt. Sengondo Mvungi, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi ambaye pia ni Mjumbe wa tume ya Katiba (pichani), amevamiwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake jijini Dar es salaam na amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiofahamika ambao habari za awali zinadai kuwa ni majambazi.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi Taifa, Mhe Moses Machali, ameiambia Globu ya Jamii muda mfupi uliopita kwamba Dkt Mvungi alijeruhiwa vibaya sana usiku (wa kuamkia leo) saa 6.Mhe Machali amesema taarifa zilizopatikana ni kwamba walimkata mapanga hasa kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu, na kwa sasa yupo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
"Wana NCCR-Mageuzi na Watanzania wote tupeane pole kwa uvamizi wa Dkt Mvungi. Tumwombee na kumtakia apate kupona haraka", alisema Mhe. Machali, ambaye pia ni Mbunge wa Kasulu Mjini, akiongezea kuwa hali yake ni mbaya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: