HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » REDDS MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA AALIKWA NCHINI UGANDA KUSHIRIKI MAONYESHO YA MAVAZI.


Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa yuko Kampala nchini Uganda kwa mwaliko rasmi kutoka kampuni ya Arapapa Fashion House & Design ya nchini Uganda.
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa atakuwepo nchini Uganda kwa muda wa siku 5 ambapo ataanza tarehe 05 hadi tarehe 09 Novemba 2013 anatarajiwa kurejea nchini.
Akiwa nchini Uganda ataungana na warembo wengine kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Kenya, Rwanda, Burundi na wenyeji Uganda.
Pamoja na mambo mengine warembo hao watahusika pia katika kazi za jamii na baadaye kupanda jukwaani pamoja katika onyesho la mavazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo.
Kampuni ya Arapapa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tangu mrembo Happiness  anyakue taji na waliazimia kumualika mrembo huyo kutembelea Uganda, jambo ambalo wamelitimiza.
Redds Miss Tanzania 2013 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa  Shahada ya Juu katika Chuo cha Strathclyde  nchini Scotland, ameamua kuahirisha masomo yake kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi hapo atakapovua taji mwishoni mwa mwaka 2014.
Mrembo Happiness Watimanywa atawakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia hapo mwakani.
HIDAN .O. RICCO.
PRO.
LINO INTERNATIONAL AGENCY LTD.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: