WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI KWENYE MSAFARA WA RAIS
Wananchi na viongozi wakitoa msaada kwenye Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja
wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari kwenye msafara wa rais
Askari akilikagua Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja
wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita.
Msafara wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete mkoani Geita, leo umeingia dosari baada ya gari moja lilokuwa kwenye msafara huo kupinduka na kujeruhi watu watano.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Geita Lenard Paul ajali hiyo imetokea leo saa 3 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Nyankumbu kilomita 3 kutoka makao makuu ya mkoa wa geita.

Kamanda
Paulo amesema gari hilo namba DFP.9730 aina ya Toyota Landcruzer lililokuwa
likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa (MSD), lilipinduka
baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani hii leo.
Amewataja
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa
ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na Radio Free Afrika, Peter
Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa
MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.
Kamanda
Paulo amesema majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita
kwa ajili ya matibabu na kisha kuruhusiwa huku Mwandishi Peter Makunga akiwa
bado amelazwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea vizuri.
Source: Faraji Mfinanga.
Source: Faraji Mfinanga.
Post a Comment