Watalii watatembela mbuga kuangalia miti baada ya kuona picha hii ya
tembo makumbusho? embu ona mbuga inavyopendeza kwa kuwa na wanyama hawa
jamani.
TEMBO waliopo nchini wanaokadiriwa kuwa sio zaidi ya 70,000 watakuwa
wamefutika katika uso wa dunia nchini kwetu miaka michache ijao endapo
hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na majangili.
Katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo kusini mwa Tanzania ambayo ni
Hifadhi ya Taifa kubwa kuliko zote nchini yenye ukubwa wa kilometa za
mraba 20,226 ina tembo zaidi ya 30,000 ,utafiti umebaini kuwa majangili
yamekuwa yanawauwa tembo hao kwa kasi hali inayotishia uwepo wa wanyama
hao ndani ya hifadhi hiyo.
Kwa uchunguzi uliobainika, baadhi ya majangili ambao walikamatwa katika
hifadhi hiyo walikutwa wakitumia silaha za kisasa zikiwemo zile ambao
zilitumika katika vita ya Idd Amini wa Uganda kati ya mwaka 1978 hadi
1979.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Utafiti ambao ulifanywa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mwaka 1985
ulibaini kuwa vitendo vya ujangili ambavyo vilikuwa vinafanywa na jamii
inayozunguka hifadhi hiyo vilisababisha idadi ya tembo katika hifadhi
hiyo kupungua kutoka tembo 2500 hadi kufikia tembo wasiozidi 500 .
Taarifa za (TANAPA) zinabainisha kuwa utafiti ambao ulifanywa mwaka
2011 unaonyesha kuwa ujangili unasababisha katika Tanzania tembo zaidi
ya 30 kufa kila siku sawa na tembo 850 kwa mwezi na tembo zaidi ya
10,000 wanauwawa kila mwaka hali inayohatarisha wanyama hao kufutika
katika Tanzania.
Takwimu zinaonyesha kuwa katika pori la akiba la Selous hadi kufikia
mwaka 2007 kulikuwa na tembo zaidi ya 70,000 hata hivyo idadi ya tembo
katika pori hilo imeshuka kutokana na kukithiri kwa ujangili hadi
kufikia tembo 43,000 mwaka 2009 ambapo hivi sasa inakadiriwa huenda
idadi ya tembo katika pori hilo imeshuka na kufikia 30,000 tu.
Shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa nchini China mwaka 2012 kutoka
hapa nchini ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni moja na
nusu. Wiki mbili kabla ya hapo takribani tani nne za meno ya Tembo
zilikamatwa huko huko HongKong katika nchi ya China.
Matukio haya mawili ya shehena za meno ya tembo ni sawa na Tembo 900
waliouwawa.Hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa ujangili umeshamiri kwa
kasi ya kutisha na kuhatarisha maisha ya wanyamapori hususani tembo.
Takwimu za Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii zinaonyesha
kuwa mwaka 2010 hapa nchini jumla ya Tembo 10,000 waliuwawa, takwimu
hizo ni sawa na Tembo 37 waliuwawa kila siku.
Kulingana na takwimu hizo hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2012 ambapo
jumla ya Tembo 23,000 waliuwawa sawa na wastani wa Tembo 63 kila siku,
kutokana na kasi hii ya ujangili, ifikapo mwaka 2018 inakadiriwa
Tanzania haitakuwa na Tembo hata mmoja.
Mimi kama mtanzania hali hii inanitisha sana ukizingatia umuhimu wa
wanyama hao hasa katika hifadhi zetu, ambapo mbali na kuongeza pato la
taifa na kuingiza fedha za kigeni pia inaipatia nchi yetu heshima ya
utalii.
Hakuna hifadhi ya aina yoyote duniani watu hutembelea kuona msitu, panya
pori (buku) wala mende bali simba, chui, tembo, mbogo n.k.
Pamoja na hatari hiyo ya kuwapoteza wanyama hawa, mimi sijawahi kusikia
adhabu wanayopewa hawa wanaokamtwa na meno ya tembo kila kukicha na kama
huwa napitiwa na taarifa hizo naomba nikumbushwe kwani tumekuwa
nimekuwa nikisikia wakikamatwa lakini adhabu yao siijui.
Ninachojiuliza, je siku tembo hawa wakipotea wao na kizazi chote watalii
wataendelea kuitaja nchi yetu kwa kuja kuangalia picha za historia za
wanyama hao maana nimehudhuria mikutano mingi ya kimataifa ambapo
wakimaliza mkutano siku ya mwisho hupendekeza kwenda mbuga za wanyama
kabla ya kurudi makwao.
CHANZO: MALIASILI ZETU

No comments:
Post a Comment