Mwimbaji wa ‘Baby’ Justin Bieber, Jumanne wiki hii alienda Ufilipino kuwatembelea watu walioathirika na kimbunga kilichosababisha wengi kupoteza maisha, pamoja na hasara kubwa kwa nchi hiyo hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Associated Press, ziara ya Bieber nchini Ufilipino ni sehemu ya jitihada za nyota huyo kutoka Canada wa kutoa misaada kwa wale waliopatwa na janga la kimbunga nchini humo.
Msemaji wa UNICEF alisema “Justin brought a lot of joy, hope and cheer to the hundreds of children who were there.”
Bieber amekuwa akiendesha kampeni ya kuwashawishi mashabiki wake wa facebook kuchangia kuwasaidia waathirika wa kimbunga kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, na mpaka sasa amefanikiwa kukusanya $600,000 katika lengo lake la kufikisha dola milioni moja ambazo zote zitapelekwa kwa waathirika hao.
Akiwa Ufilipino Bieber aliwafariji kwa kutoa misaada mbalimbali kwa watoto na kufanya show maalum.
No comments:
Post a Comment