HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MFANYAKAZI WA CBE -DODOMA AFARIKI DUNIA LEO

 MAREHEMU SELINA MAKINGI (MAMA ADAM)
 
Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Elimu ya Biashara  (CBE) Kampasi ya Dodoma  (COBESO)  Imepokea taarifa za kifo cha  Mfanyakazi wa Chuo  Marehemu  Selina Makingi  (Mama Adamu) kwa masikitiko makubwa.

Kwa niaba ya Wanafunzi  wote  Rais wa Serikali ya Wanafunzi  CBE  - Dodoma  Mh. Remidius M. Emmanuel   anatoa pole kwa  Wafanyakazi wote  wa Chuo cha CBE  pamoja na ndugu jamaa na Marafiki  waliofikwa na Msiba huo.

Taarifa za Msiba huu  zimeifikia  Serikali ya  COBESO   Mapema Asubuhi ya Leo (27/12/2013)  kutoka kwa Kaimu  Afisa Mwandamizi Rasilimali watu na Utawala  Bi. Msemo, N .  Ambaye kupitia taarifa yake amesema  Bi. Selina  Makingi  Amefariki  leo Asubuhi Desemba 27, 2013 katika Hospitali ya Mkoa Dodoma, na kuongeza kuwa   Taratibu nyingine za msiba  zitaendelea kutolewa.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA.

JINA LA BWANA  LIHIMIDIWE

AMINA.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: