Kunenepa kupindukia ni tatizo ambalo sasa linatishia
zaidi maisha ya wengi katika mataifa yanayostawi duniani kuliko katika
mataifa tajiri ambako mambo yana afadhali.
Sasa serikali nyingi zinaombwa kuongeza Ushuru
vyakula hivyo vinavyosababisha watu kunenepa kupindukia kama njia ya
kuokoa maisha ya watu kutokana na mshutoko wa moyo, kisukari na kiarusi.
Kutokana na takwimu za kimataifa, kila mtu mmoja kati ya watatu
wazima duniani, anatambuliwa kama aliyenenepa kupita kiasi. Mwaka 1980
takwimu hiyo ilikuwa kila mtu mmoja kati ya watano.
Ripoti ya Shirika la utafiti wa matumizi ya
chakula la The Future Diets, lilikagua takwimu zilizopo na kugundua kuwa
ongezeko la watu wanene kupindukia limetokea katika mataifa yanayostawi
kama vile Mexico na Misiri, ambako watu wanatumia utajiri wao wa ziada
kula vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi.
Katika muda huo idadi ya wanene ilipanda mara tatu kutoka Milioni 250 hadi Milioni 904.
Ripoti hiyo inasema kwamba mataifa yaliyostawi
ambayo yamekuwa na changa moto nyingi zaidi kuhusiana na maswala ya
unene yameshindwa kuthibiti kikamilifu maswala yanayohusiana na hali
hiyo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Ripoti hiyo imemulika kampeni iliyofaulu nchini
Korea Kusini ambako wanawake wanafunzwa jinsi ya kutengeneza vyakula
kiasili ambapo mafuta madogo zaidi yanatumika.
Wanawake wawili waliopatikana katika kibanda cha
kuuza matunda katika mji mkuu wa Korea Kusini wa Seoul waliambia BBC
sababu za wembamba wao. Mmoja alisema hana wasiwasi wa kunenepa kwa
sababu yeye hupenda kunywa uji, mboga na matunda.
Mwanamke wa pili alisema kuwa raia wengi wa
Korea wanapenda mboga zaidi, ambapo wenzao kutoka mataifa ya Mahgaribi
hupendelea kula nyama ya Ng'ombe. Mama huyo alisema pia kuwa kwa kawaida
raia wa Korea kwa ujumla hula chakula kidogo zaidi kwa sababu wanajali
zaidi unene wao.
Ripoti hiyo inapendekeza kuwa mataifa mengi yanapaswa kutoza kodi kubwa vitamutamu kama vile soda na peremende.
Ripoti hiyo ya The Future Diets inasema kuwa
iwapo mienendo ya ulaji wa sasa itaendelea kutakuwepo na ongezeko zaidi
la mshtuko wa moyo, kiharusi na ugonjwa wa sukari.
BBC SWAHILI




No comments:
Post a Comment