Bunge Maalum la Katiba Limekutana Jioni Hii kuendelea na Shuguli zake Lakini Mvutano Mkubwa Umejitokeza Hali iliyosababisha Vurugu Iliyoambatana na Kuzomea Zomea,Mvutano Huo Uliibuka Pale Mjumbe Mh Tundu Lissu Aliposimama kuomba Muongozo Kuhusu Marekebisho ya Kanuni Ambayo Tundu Lissu anamtuhumu Mwenyekiti wa Bunge Mh Samweli Sitta Kupitia Kamati ya Uongozi kuleta Marekebisho Ya Mabadiliko ya Kanuni Kinyume cha Kanuni zilizopitishwa na Bunge Hilo la Katiba Wakati wakijadili na Kupitisha Kanuni za Bunge Hilo.
Mwenyekiti wa Bunge Hilo Mh Samwel Sitta Aliingilia Kati kujaribu Ufafanuzi Pamoja na Wajumbe Wengine Akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh Jaji Fredrik Warema Lakini
hali ya Kuzomea Iliendelea Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Hilo Alipolazimika
Kuliahirisha Bunge Hilo Mpaka Kesho na Kuamuru Mapendekezo ya
Mabadiliko HayoMabadiliko hayo Yapelekwe kwenye Kamati Ya Kanuni Kajili
ya Maamuzi ili Yaweze Kuwasilishwa Katika Bunge Hilo.
No comments:
Post a Comment