Yanga wakishangilia bao la Didier Kavumbagu (wa pili kulia) lililopelekea mauti ya Deodatus Lusinde.
SHABIKI wa Timu ya Yanga SC, Deodatus Isaya Lusinde, mkazi wa Kipunguni A, amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla wakati akishangilia bao la Yanga lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza.
Marehemu amepoteza maisha akiwa chumba cha matibabu mara baada ya kuwekewa mashine ya oksijeni na taarifa kuhusu kifo cha shabiki huyo zimethibitishwa na mmoja wa madaktari aliyemhudumia akiwa uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor Matuzya.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Bwana Isaya alikuwa Meneja wa Bar ya Rose Hill iliyopo Segerea jijini Dar. Ameacha mke aitwaye, Rose William Lusinde ambaye ni askari magereza.
Marehemu amekutwa na mauti hayo wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya timu yake ya Yanga na Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mungu ailaze roho ya mwanamichezo, Deodatus Isaya Lusinde mahali pema peponi. AMEN!
No comments:
Post a Comment