Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
wakiwashangilia kwa lugha ya alama wajasiriamali wenye ulemavu wa
kusikia (hawapo pichani) wakati wakijitambulisha kwenye semina
iliyoandaliwa na TBS kwa ajili ya kuwafunda walemavu hao masuala ya
viwango vya ubora katika shughuli za,uzalishaji.
Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwasisitizia walemavu wasiosikia
(viziwi) kuzingatia ubora wa viwango kwenye bidhaa wanazozalisha kwenye
sekta ya kilimo, ufugaji nyuki na mifugo na ujasiriamali ili kunufaika
na masoko ya kimataifa wakati akifungua semina kwa walemavu hao juu ya
masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango
tanzania TBS, semina hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma, wengine pichani
ni maafisa kutoka TBS.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Afisa uhusiano wa taasisi ya maendeleo ya viziwi tanzania ndg.
Nicholaus Lubinga (aliyesimama nyuma) akizungumza jambo kwa lugha ya
alama wakati wa semina ya masuala ya viwango vya ubora kwa
wwjasiriamali wenye ulemavu wa kusikia iliyoandaliwa na TBS ambayo
imefanyika mjini dodoma.
Wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia viziwi wanaojihusisha na shughuli
za uzalishaji katika sekta za kilimo, mifugo na nyuki na ujasiriamali
kutoka mikoa ya Dodoma singing, tabora na shinyanga wakisikiliza kwa
makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa Dodoma na
kutafsiriwa kwa lugha ya alma wakati wa ufunguzi wa semina ya masuala ya
ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na
kufanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) wanaojihusisha
na shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, ufugaji mifugo na
nyuki na ujasiriamali kutoka mikoa ya Dodoma, singida, Tabora na
shinyanga wakishangilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mkuu wa mkoa
Dodoma na kutafsiriwa kwa lugha ya alama kwenye semina ya masuala ya
ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS mjini Dodoma.
Picha ya pamoja baina ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi, wataalamu wa masuala ya viwango vya ubora kutoka TBS na walemavu wasiosikia (viziwi) kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua semina kwa walemavu hao juu ya masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na kufanyika mapema siku ya Jumatatu Machi 24, 2014.








No comments:
Post a Comment