Mkuu wa Mkoa
Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akifanya ukaguzi wa vitabu na nyaraka za taarifa mbalimbali
kwa ajili ya wasomaji , pembeni yake ni Mkutubi msaidizi wa maktabaa hiyo
Ndg. Judith Lugongo, ukaguzi huo ulifanyika mapema Leo hii wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye
kilemba kichwani) akikagua jengo la maktaba mkoa wa Dodoma kujionea
mfumo wa vifaa vinavyotumika kutolea elimu na taarifa mbalimbali kwa
njia ya video na sauti, zoezi hili la ukaguzi lilifanyika mapema leo
kwenye viwanja vya maktaba ya Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya
bodi ya huduma za maktaba.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Watumishi wa maktaba ya mkoa Dodoma wakiwa tayari
kupokea wananchi wenye mahitaji mbalimbali ya huduma za maktaba kwa
ajili ya kuwapa maelekezo ya namna ya kupata taarifa na huduma nyingine
mbalimbali mapema leo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya
huduma za maktaba, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya
maktaba ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr
Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akikagua nyaraka na vitabu
mbalimbali wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya vitabu wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba Nchini, maadhimisho
mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba ya mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye
kilemba kichwani) akipata ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa kutafsiri
taarifa za vitabu na nyaraka mbalimbali katika lugha za watu wenye
mahitaji maalumu/wenye ulemavu wa kuona (nukta nundu) Mwl. Charles
Mtimatuku mapema wakati anatembelea mabanda ya maonesho wakati wa
hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini
mkoani Dodoma. Huduma za maktaba nchini zimepiga hatua kiasi cha
kuzalisha taarifa na nyaraka mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu.
No comments:
Post a Comment