NAKUMATT KUZINUNUA SHOPRITE ZA TANZANIA KATIKATI YA MWAKA HUU, SABABU YA SHOPRITE KUONDOKA TANZANIA YATAJWA


Wamiliki wa msululu wa supermarket kubwa za Kenya, Nakumatt, watatakiwa kusubiri hadi katikati ya mwaka huu kabla ya kununua supermarket tatu za kampuni ya Shoprite ya Afrika Kusini zilizopo nchini.
Manunuzi hayo yalitakiwa kufanyika mwezi huu wa nne lakini sasa yatafanyika baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa tume ya ushindani Tanzania, FCC. “Hatuna uhakika lini tutachukua maduka hayo kwakuwa tumeambiwa na tume ya ushindani ya Tanzania kungoja kwa miezi mitatu mingine,” alisema Thiagarajan Ramamurthy, Head of Strategy and Operations wa Nakumatt.
Sababu za kuchelewa huko hazijatajwa.
Supermarket hizo zitauzwa kwa gharama ya dola milioni 40.45. Nakumatt imeahidi kuwaajiri wafanyakazi wa Shoprite pale itakapozinunua ili kupunguza gharama ya kuajiri wafanyakazi wapya. Kampuni hiyo ya Afrika Kusini inaondoka Tanzania baada ya kuonywa kuacha kuchukua bidhaa kutoka Afrika Kusini na kutopromote zile za Tanzania.
Kwa upande wake Nakumatt imepanga kuwapa kipaumbele wazalishaji wa bidhaa wa Tanzania na wale wa Kenya waliopo Tanzania. Hatua hiyo ya kuchelewashwa kwa manunuzi hayo kunaiathiri Nakumatt ambayo ilikuwa imejipanga kuanza biashara mwezi huu. 

No comments

Powered by Blogger.