Zikiwa zimebaki siku nane kutoka kwa movie ya Zena na Betina kumetokea tofauti kati ya Gazeti la Sani na Nisha's Film Production. Gazeti hilo liliweka pingamizi ya kutokutoka kwa movie hiyo wakidai filamu hii imetumia majina yao ambayo ni "Zena" na "Betina" lakini mpaka sasa maongezi yanendelea na makubaliano yako kwenye hatua ya mwisho ili Movie hiyo iweze kutoka kwa wakati uliopangwa.
Movie hii inagonga vichwa vya wengi kwani inakuja kitofauti hivyo inaweza kuweka record kwenye mauzo yake sokoni. Filamu hii waliocheza Senga, Salma Jabu na Hanifa Daudi inategemea kuingia sokoni May 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment