Tunapoutizama ulimwengu, kila mtu anataka maisha mazuri na wakati mwingine unakaa kujiuliza maisha hayo mazuri ni yapi? Katika Tanzania hii tumechanganya maisha mazuri na kuwa na fedha nyingi au utajiri. Na imetupelekea vijana wengi tukaanza kufanya vitu vya ajabu ili tuwe na maisha mazuri bila kujua hayo maisha mazuri ni yapi? Inategea na uelewa wako wa mambo na sehemu ambayo ulilelewa.
Maisha mazuri ni pale ambapo unaridhika na kile ulichonacho,kupata mahitaji ya msingi ya kibinadamu kulingana na eneo ulilopo. Mfumo wa maisha unabadilika kila siku, na tumekuwa na tafsiri tofauti tofauti kuhusu maisha mazuri bali ukweli wa mambo ni kwamba ukishindwa kuridhika na kufuruahia ulichonacho sasa itakuwa ngumu kujua kama unamaisha mazuri. tatizo litakuja pale unapotaka kujilinganisha na watu wengine au marafiki zako na unajikuta unaanza kuishi kulingana na watu wengine au marafiki zako wanavyotaka au kuelezea maisha mazuri.
Kuna watu walifikiri watu wenye maisha mazuri ni wale wanakaa na kunywa na wao wakaanza kunywa na cha kushangaza, wamejikuta familia zao zikisambaratika kwa sababu ya yeye kuwa mlevi n.k. Unapotafuta maisha mazuri inabidi uanzie na mambo ya msingi kibinadamu, halafu mengine yanafofuata ni ziada au anasa. Ukiweza kula, ukapata nyumba ya kuishi au mahali pa kuishi na maji tayari unaweza kuishi maisha mazuri. Na huo ndio msingi wa maisha ya mwanadamu. Unaweza ukakubali au ukakataa ila ukweli wa mambo unabaki palepale, je wewe maisha mazuri kwako ni yapi?
Mara ngapi tumeingia kwenye matatizo tukitafuta maisha mazuri? Je umegundua unachokuwa unakitafuta ni ziada tu?
No comments:
Post a Comment