HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU FROSSIE CHIYAONGA ALIYEKUWA BALOZI WA MALAWI NCHINI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili huo unatarajia kusafirishwa kuelekea Malawi kwa maziko
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII WA KUBOFYA HAPA CHINI

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji baadhi ya wanandugu na familia ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Malawi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania.
 Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.


 Sehemu ya waombolezaji mabalozi wa nchi mbalimbali waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Picha na OMR

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: